Ukaguzi wa kundi la nyuki

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=tlqXDInZUoE

Muda: 

00:10:12
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

University of Guelph Honey Bee Research Centre
Katika ufugaji wa nyuki, ukaguzi wa makundi humsaidia mfugaji kujua hali halisi ya mzinga.
Ili kufanya ukaguzi wa kundi la nyuki, puliza moshi kwa mzinga na kisha uufungue. Wakati wa ukaguzi, tunaangalia ishara na hali zote ambazo mzinga wa kawaida unapaswa kuwa nazo, na wakati huo huo tunaangalia ishara za magonjwa.

Jinsi ya kukagua

Kata na uondoe polepole kiunzi cha kwanza cha mzinga. Katika kiunzi hicho, unapaswa kuona asali iliyohifadhiwa, chavua mbichi kwenye masega yanayong’aa, na nyuki dalili ambayo inamaanisha kiunzi hicho lazima kina akiba ya chakula.
Egemeza kiunzi hicho kwenye kona ya mzinga na uondoe kiunzi kifuatacho ili kuendelea kukagua. Hiki kinaweza kuwa na nyuki,viwavi, na mayai. Ili kuona mayai hayo, weka mkono wako kwenye kiunzi ili kuwaondoa nyuki na ushikilie fremu hivi kwamba mwanga wa jua uangaze moja kwa moja chini ya kiunzi.
Wakati wa ukaguzi, kumbuka kuwa viwavi vya nyuki kibarua huwa na masega yenye nyumba zilizotambarare, huku viwavi vya nyuki dume wana masega yenye nyumba zilizo na umbo la duara juu yazo. Wakati hali ya hewa ni ya joto, gundi ya nyuki (propolis) huwa laini na viunzi ni rahisi kuondolewa. 
Malkia atapatikana mahali ambapo kuna masega yenye nyumba nyingi zilizo wazi ambapo anaweza kuwa anataga mayai katika kiota cha majana. Upande wa juu wa sega
huhifadhiwa chavua na sehemu ya chini ya sega
huhifadhiwa asali.
Kila mara rejesha kila kiunzi mahali pake baada ya ukaguzi.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:12Ili kufanya ukaguzi wa kundi la nyuki, puliza moshi kwa mzinga na kisha uufungue.
01:1302:10Kata na uondoe polepole kiunzi cha kwanza cha mzinga.
02:1104:24Egemeza kiunzi hicho kwenye kona ya mzinga na uondoe kiunzi kifuatacho ili kuendelea kukagua.
04:2506:50Tofauti kati ya kiwavi cha nyuki kibarua na cha nyuki dume
06:5109:00Malkia atapatikana mahali ambapo kuna masega yenye nyumba nyingi zilizo wazi
09:0110:00 Kila mara hurejesha kila kiunzi mahali pake baada ya ukaguzi.
10:0110:12Hitimisho

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *