Biringanya ni mboga ladha na yenye lishe, na hukuzwa kwenye aina zote za udongo mwaka mzima.
Mavuno mengi zaidi hupatikana wakati wa majira ya baridi, kwani majira haya huhimiza ukuaji zaidi wa maua pamoja kupunguza matukio ya magonjwa. Kawaida biringanya huathiriwa sana na magonjwa na minyoo ambayo husababisha mavuno kidogo.
Kupanda biringanya
Andaa miche kabla ya kupanda, na panda kulingana na aina. Tengeneza mifereji ya maji na mitaro kati ya safu ili kuondoa maji ya ziada. Kabla ya kupanda, lima ardhi mara 4-5 ili kuboresha muundo wa udongo. Weka mbolea za kikaboni na mbolea za madini kwa wakati ufaao ili kuboresha kiwango cha rutuba ya udongo. Mwagilia mashamba maji na dhibiti wadudu waharibifu wa mimea.
Usimamizi wa mazao
Dhibiti ugonjwa wa mnyauko ambao una sifa ya kunyausha majani, kudondosha matunda na kuua mmea. Usihifadhi unyevu mwingi shambani, na pia usilime aina hiyo hiyo ya biringanya kila msimu ili kusaidia kudhibiti mzunguko wa maisha ya ugonjwa. Zungushia shamba uzio wa wavu ili kuzuia mashambulizi ya ndege. Mwishowe, palilia kila mara, lainisha udongo uliokuzunguka mimea, na vuna katika wakati sahihi ili kuepuka hasara kutokana na wanyama pori na wezi.