Ukingo wa mito hulindwa kwa kupanda mimea kwenye ukingo, pamoja na maeneo yaliyo karibu na mito. Hii hudhibiti mmomonyoko wa ukingo, mporomoko wa ardhi na mtiririko wa mchanga katika mto.
Daima ni muhimu kwa wakulima kulinda kingo za mito kwa sababu huku kunazuia mmomonyoko wa ardhi, kunapunguza mtiririko wa maji na uharibifu wa mafuriko, na kuboresha maisha ya mkulima kwa sababu miti iliyopandwa hutoa kuni, mbao, lishe ya wanyama na matunda kwa familia.
Hatua za kupanda
Panda nyasi za napier katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kwani nyasi hustawi na hivyo kutunza udongo dhidi ya mmomonyoko.
Pia panda, miti ya mgrivea lakini usijaze shimo la kupandia na udongo ili liweze kukusanya maji yanayotiririka.
Panda miti ya mpera ukingoni mwa mito ikiwa ukingo umethibiti vyeme. Hizi hufanya msitu mzuri wa kulinda udongo, matunda yake yanaweza kuliwa na pia ni chanzo kizuri cha kuni.
Unaweza pia kupanda miti ya mianzi kwa ukingo ambapo kuna mtiririko wa mto wa nguvu.
Linda miti ya asili kwa sababu huwa inahifadi udongo na kudhibiti mmomonyoko.
Mwishowe tunza kingo za mito kupitia udhibiti wa magugu, kukata nyasi ya napier na kupogoa miti.