Kwa ajili ya ongezeko la ukuaji wa miji, kuna haja ya kujumuisha upandaji wa miti katika mazingira yetu ya mijini.
Hatua ya kwanza ya kuanzisha misitu katika mazingira ya mijini ni kutambua miti ambayo ni asili ya mkoa huo, na kuikuza kwa uangalifu katika viriba vilivyojazwa udongo wenye rutuba, samadi ya ng’ombe na mbolea ya nazi. Vichaka vinapaswa kupandwa kando ya miti.
Uanzishaji wa misitu mijini
Tayarisha ardhi kwa ajili ya kupanda. Kuku kunafanywa kwa kuondoa mawe na miamba kutoka eneo la kupandia. Samadi ya ng’ombe, na mbolea ya nazi huchanganywa vizuri na udongo kwa uwiano wa kilo 10 kwa kila mita ya mraba.
Weka miche kwenye eneo ambapo itapandwa kwa angalau wiki 2. Huku kunawezesha miche kuzoea hali mpya ya hewa na mazingira.
Panda miche 4 kwa kila mita ya mraba. Huku kunawezesha miche kukua haraka. Miti, vichaka na mimea ya kutambaa vinapaswa kukuzwa pamoja kama vilivyo katika msitu halisi. Jaribu kupanda angalau mimea 400 ya aina 100 katika eneo dogo la mita 100 za mraba.
Kupalilia kunaweza kufanywa ili kuhifadhi unyevu wa ardhi. Ongeza mbolea za kikaboni ili kuongeza ukuaji wa haraka.