Upungufu wa kalsiamu katika ng’ombe wa maziwa

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/calcium-deficiency-dairy-cows

Muda: 

00:15:29
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Access Agriculture
Malisho ni mojawapo  ya sababu kuu zinazoathiri ufanisi wa uzalishaji wa mifugo kuhusiana na ubora na wingi wa bidhaa.
Kwa vile wakulima wanakosa malisho bora ya mifugo kutokana na ukosefu wa nyasi za kutosha, mifugo huathiriwa sana na upungufu wa kalsiamu, jambo ambalo husababisha ukuaji duni, huchelewesha utoaji wa maziwa na husababisha uzazi duni. Hii huathiri zaidi ng’ombe wa maziwa.

Upungufu wa madini

Viwango vidogo vya kalsiamu katika mwili wa mnyama hudhoofisha mifupa. Upungufu wa kalsiamu husababisha homa ya maziwa kwa ng’ombe. Katika hali hiyo, wasiliana na daktari wa mifugo ili kumdunga ng’ombe dawa ya kalsiamu la sivyo atakufa. Ng’ombe huhifadhi kalsiamu kwenye mifupa.
Vile vile, kalsiamu hupatikana kutoka kwa jamii ya kunde hivyo basi wape ng’ombe kilo 2 za malisho ya kunde, malisho ya mahindi na sileji kila siku. Wape wanyama majani yenye kalsiamu mara mbili kwa wiki, na kisha loweka mbegu za pamba usiku kucha na mpe kila ng’ombe nusu kilo kila siku. Mpe kila ng’ombe kilo 2 za nyasi baada ya kukamuliwa na apate chakula cha kutosha wakati wa kiangazi.
Endelea kwa kumpa ng’ombe mjamzito kilo 2 za chakula kilichosawazishwa katika miezi 3 ya ujauzito kabla hajazaa. Baada ya kuzaa mpe ng’ombe 250 g ya chakula kilichosawazishwa. Changanya kilo 1 ya unga wa mtama na sukari ya kahawia na mpe ng’ombe baada ya kuzaa. Mwezi mmoja baada kuzaa, mpe majani machungu kila siku.
Changanya unga wa maganda ya mayai kwenye maji na malisho, na mpe ng’ombe. Weka 1/2 kg ya unga wa chokaa ndani ya chombo na uchanganye na lita 5 za maji na acha mchanganyiko hadi usiku kucha. Wakati wa asubuhi, mimina tu safu ya juu ya maji safi ya chokaa kutoka kwenye sufuria.
Hatimaye, changanya maji haya na malisho, na mpe ng’ombe na pia waweza kuwasiliana na daktari wa mifugo iwapo hali ya mnyama ni mbaya.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:39 wakulima wanakosa malisho bora ya mifugo
00:4000:59Upungufu wa kalsiamu husababisha ukuaji duni, huchelewesha utoaji wa maziwa na husababisha uzazi duni.
01:0001:32Viwango vidogo vya kalsiamu katika mwili wa mnyama hudhoofisha mifupa na hupunguza uzalishaji wa maziwa
01:3301:43 Upungufu wa kalsiamu husababisha homa ya maziwa kwa ng'ombe
01:4402:31 wasiliana na daktari wa mifugo ili kumdunga ng'ombe dawa ya kalsiamu
02:3202:52Ng'ombe huhifadhi kalsiamu kwenye mifupa.
02:5304:03 Upungufu wa kalsiamu husababisha homa ya maziwa kwa ng'ombe
04:0405:33Mpe ng'ombe silaji, lishe ya mahindi na majani yenye kalsiamu nyingi mara mbili kwa wiki.
05:3406:20 loweka mbegu za pamba usiku kucha na mpe kila ng'ombe nusu kilo kila siku.
06:2107:34 Mpe kila ng'ombe nyasi baada ya kukamuliwa na mpe chakula cha kutosha wakati wa kiangazi.
07:3507:58Mpe ng'ombe mjamzito chakula kilichosawazishwa katika miezi 3 ya ujauzito kabla hajazaa.
07:5909:09Baada ya kuzaa mpe ng'ombe chakula kilichosawazishwa.
09:1009:36Changanya unga wa mtama na sukari ya kahawia na mpe ng'ombe baada ya kuzaa
09:3710:02Mwezi mmoja baada kuzaa, mpe majani machungu kila siku.
10:0312:07Changanya unga wa maganda ya mayai kwenye maji na malisho, na mpe ng'ombe.
12:0812:20Weka unga wa chokaa ndani ya chombo na uchanganye na lita 5 za maji
12:2112:25Wakati wa asubuhi, mimina tu safu ya juu ya maji safi ya chokaa kutoka kwenye sufuria.
02:2613:08Changanya maji haya na malisho, na mpe ng'ombe na pia waweza kuwasiliana na daktari wa mifugo
13:0915:29Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *