Upunguzaji wa miti ni jambo muhimu katika usimamizi wa misitu.
Upunguzaji wa miti hufanywa ili kuwezesha miti bora zaidi kukua vizuri na pia kuruhusu mwanga wa jua kupenya kupitia matawi hadi ardhini, na kuruhusu ukuaji wa mimea ardhini. Katika upogoaji wa miti, kuna miongozo ambayo inapaswa kufuatwa, na hii huamua juu ya mti gani inayopaswa kuondolewa na ni upi utakaoachwa shambani.
Uchaguzi wa miti
Ili kujua ni mti gani wa kuondoa shambani, unaweza kutumia kanuni ya jumla ambapo unaondoa mti mmoja kati ya miti mitatu. Hii haimaanishi kwamba unaondoa kila mti wa tatu mfululizo kihisabati.
Wakati wa kuchagua miti ya kuondolewa, uwe na panga ambalo hutumika kuweka alama kwenye miti ambayo itaondolewa. Uwekaji alama hufanywa kwa kukata mikato katika pande zote mbili za mti ili mkata-miti atambue kwa urahisi ni miti gani ya kukatwa na ni ipi ya itakayoachwa.
Wakati wa upunguzaji miti, unashauriwa kuanza na miti iliyoinama, miti iliyokufa na ile inayozuia ukuaji wa miti inayopendekezwa. Baada ya kuchagua miti hiyo, miti zaidi inaweza kuchaguliwa ili kufikia kanuni ya jumla ya kuondoa mmoja katika kila miti mitatu.
Baada ya kuweka alama kwenye miti, unaweza kuamua kuiuza kwa mkandarasi