Ndama huhitaji usimamizi mzuri ili kukua vyema, kwa hivyo wafugaji wanapaswa kuzingatia kanuni za kimsingi za usimamizi ili kuongeza uzalishaji.
Ulishaji sahihi wa ndama huwasaidia kukua wakiwa na afya njema, pamoja na kufikia ukomavu wa mapema wa kijinsia. Hii huongeza kipato endelevu na bidhaa bora za mifugo. Kwa hiyo, inapendekezwa kila mara kwa wakulima kufuata taratibu hizi za usimamizi.
Mbinu za usimamizi
Daima walishe ndama maziwa ya kwanza (kolostramu) katika siku za kwanza ili kuongeza kinga ya ndama dhidi ya magonjwa, kisha walishe ndama ukitumia chupa.
Pili, mfunze ndama kulishia kwenye ndoo ili aweze kunywa maziwa mazuri kwa kiwango cha moja ya kumi ya uzito wa mwili wake.
Wape ndama chakula cha kuanzia wakiwa na umri wa siku 15 hadi miezi 3 ili kuongeza kiwango cha nishati na pia kuboresha ukuaji wa tumbo.
Baada ya miezi 3 wape ndama chakula cha mkusanyiko cha kutosha ili kuongeza viwango vya nishati.
Mwisho, wape ndama mchanganyiko wa madini na virutubisho vya vitamini kwukuaji wa jumla na pia wape maji safi ya kunywa.