Usimamizi wa matawi huboresha mavuno ya kahawa. Hii ni pamoja na kupinda mashina, kupogoa, kukata machipukizi na kurejesha upya zao.
Katika Kupogoa, tunazingatia sehemu fulani ya mti ili ustawi na utoe mavuno mengi ya ubora wa juu. Hii hufanywa mara moja kwa mwaka. Kupogoa huboresha ukubwa wa tunda la kahawa na kurahisisha uvunaji wa matunda yaliyoiva. Kupogoa pia husaidia katika udhibiti wa wadudu na magonjwa, huhimiza utoaji wa maua kwa kuwezesha upenyaji mzuri wa mwanga wa jua na hewa. Kupogoa husaidia kudumisha uwiano sahihi wa majani na mazao, pamoja na uhifadhi wa maji kwenye mmea.
Hatua nyigine
Kurejesha upya mimea huanza miaka 6 hadi 7 baada ya kupanda kwa sababu katika hatua hii, mikahawa haitowi matunda vizuri. Hatua hii hupangwa miaka miwili kabla ya kuondoa mimea mama. Hii hufanywa kwa kukata kisiki cha mti, na hivyo kuruhusu machipukizi kukua. Iwapo machipukizi yamefika urefu wa takriban sm 45, kata baadhi yao huku ukiacha tu machipukizi 4 hadi 5 yaliyotenganishwa kwa muachano sahihi. Kabla ya mvua, chagua machipukizi 2 tu ambayo yatakua mashina, huku ukiondoa mengine.
Kata shina mmoja kuu kila mwaka kwa pembe ya nyuzi 45 huku mkato ukiangalia nje.
Pia, mashina yote yanaweza kukatwa mara moja na kuacha tu chipukuzi moja. Kupitia kurejesha upya, matawi hukua haraka na sawa. Hii hufanywa katika maeneo mbali mbali ya shamba ili kuepuka hasara ya mazao kwa ujumla.
Usimamizi wa matawi huboresha ukubwa wa kahawa, ubora wa mazao na huongeza mapato.