Usalama wa kibayolojia wa shamba la samaki unahusisha hatua za kudhibiti na kulinda samaki dhidi ya uvamizi wa vijidudu hatari vinavyoweza kushambulia na kuua samaki, na kusababisha hasara.
Utekelezaji sahihi wa hatua mbalimbali za usalama husaidia kudhibiti hasara zinazotokana na vifo vya samaki. Kudibiti ufikiaji ovyo wa watu kwenye eneo la kufugia samaki ni muhimu sana katika udhibiti wa uenezaji wa magonjwa shambani. Kwa kawaida kutekeleza hatua za udhibiti wa uenezaji wa magonjwa huongeza faida ya shamba.
Kudibiti ufikiaji ovyo wa watu kwenye eneo la kufugia samaki
Kwanza, wageni wote lazima waoge na kubadilisha nguo kabla ya kuingia shambani ili kuzuia kuingiza viini vya magonjwa kutoka kwa shamba lililotembelewa awali. Pia wageni wa mashambani wa kimataifa wanapaswa kukaguliwa kwani hawa wana hatari kubwa ya kuhamisha magonjwa kutoka shamba moja hadi jingine. Zaidi ya hayo, tathmini hali ya jumla ya usafi wa wageni kabla ya kuwaruhusu kufikia shamba.
Daima, usiruhusu wageni wanaokuja shambani pamoja na wanyama wao wa kipenzi kwani wanyama kipenzi wanaweza kuwa na magonjwa yanayosababisha vimelea hatari, na pia wageni wa shamba wanapaswa kufanya miadi mapema kabla ya kutembelea shamba ili kusaidia wasimamizi wa shamba kuandaa hatua za usafi wa shamba zinazohitajika. Mwishowe, hakikisha kwamba wageni wa shamba wanafuata kikamilifu sheria za shamba zilizowekwa.