Katika uzalishaji wa mahindi, kuna hatua kadhaa zinazotakiwa kufuatwa tangu wakati wa kuota hadi kuvuna ili kupata mavuno mazuri.
Wakati wa kuandaa shamba, pima udongo ili kubaini ni kiasi gani cha mbolea kinachohitajika. Acha mabaki ya mazao shambani ili kuongeza rutuba ya udongo, na tandaza udongo. Epuka kuchoma vichaka kwani hii husababisha uharibifu mkubwa kwa mazingira na udongo. Usichimbe sana udongo unapotayarisha ardhi. Tumia mbegu bora na aina zinazofaa kwa mazingira na mahitaji yako.
Mambo yanayoathiri uzalishaji
Aina iliyopandwa huathiri uzalishaji wa mahindi. Aina zinazokomaa mapema huwa na majani machache na hustawi vyema kuliko aina zinazochelewa kukomaa.
Misimu ya kupandia na hali ya hewa; wakulima wanashauriwa kupanda mwanzoni mwa mvua.
Virutubisho muhimu. Ni muhimu kuelewa hali ya rutuba ya udongo ili uweke mbolea inayohitajika kustawisha mazao katika hatua zote.
Hatua muhimu za ukuaji
Hatua ya kuibuka au kuota. Hii hutokea wiki 1 baada ya kupanda. Kina cha kupandia, uwezo wa mbegu kuota, na mvua huamua uotaji wa mbegu.
Hatua ya kutoa majani. Hii hutokea siku 30 hadi 35 baada ya kupanda na hufuatiwa na kuchanua maua na hariri.
Uchavushaji: Ufanisi wa uchavushaji huathiriwa sana na hali ya hewa. Katika hatua hii, mahindi huanza kutoa hariri. Ukame unaweza kunyausha hariri na chavuo ambayo husababisha gunzi duni na fupi.
kujaza nafaka; ni hatua ya mwisho muhimu ambayo huanza baada ya uchavushaji. Ukame, joto kali, magonjwa na upungufu wa virutubisho unaweza kuathiri mavuno.
Hatua ya ukomavu; majani na hariri hukauka. Uvunaji hufanywa katika hatua hii.