Katika nchi zinazoendelea, ndege wanaofugwa zaidi ni kuku wa kienyeji. Hata hivyo, kideri ni moja wapo ya magonjwa yanayowakabili kuku.
Katika nchi hizi, milipuko ya kideri hutokea mara moja au mbili kila mwaka na huua wastani wa asilimia 70 hadi 80 ya idadi ya kuku ambao hawajachanjwa. Mbinu za jumla zinazotumiwa kudhibiti kideri ni pamoja na; kudumisha usafi, kutoleta ndege wapya wakati wa matukio makubwa ya magonjwa, kuzika ndege wote waliokufa. Hata hivyo, mbinu bora zaidi ni kutoa chanjo.
Changamoto za chanjo
Kuna changamoto nyingi zinazokabili udhibiti wa kideri kwa kutumia mbinu ya chanjo, hasa kwa chanjo maalum ambazo lazima zihifadhiwe katika halijota ya nyuzi 2 na 8.
Idadi kubwa ya ndege lazima wawekwe pamoja katika kikundi ili kupata ufanisi na jambo la kuchanja. Yaani, chanja ndege wa umri mbalimbali kwa sababu kwa kawaida wanakuzwa pamoja.
Pia unahitaji vifaa maalum kama vile jokofu ili kuhifadhi na kutunza chanjo vizuri, jambo ambalo ni gharama kubwa.
Uchaguzi wa chanjo
Kuna chanjo nyingi za kideri na chaguo linapaswa kutegemea ufanisi wa chanjo, uwezo wa chanjo kustahimili joto, urahisi wa kutumia, usafirishaji, gharama, uwezo wa kumudu na upatikanaji katika eneo hilo. Chanjo ya aina ya I-2 huwakinga ndege dhidi ya kideri kwa ufanisi ikitumiwa kila baada ya miezi 4.
Mradi bora wa ku chanja ndege lazima ujumuishe watoa maamuzi wakuu, wafugaji, wachanjaji wa jamii, wakala wa ugani, watoa huduma wa mifugo, wafanyabiashara binafsi, wanasayansi ya kijamii au wa mifugo na mashirika yasiyo ya kiserikali.