Mifumo ya biogas haikomei kwenye matumizi ya samadi ya ng‘ombe pekee. Taka za jikoni kama vile maganda ya viazi, maganda ya mayai na mabaki ya chakula yanaweza kutumika katika utengenezaji wa gesi asilia.
Uwekaji wa samamdi ya ng‘ombe kwenye mfumo wa gesi asilia unaweza kufanywa mara moja au mbili kwa wiki, na kisha taka za jikoni zikatumika.
Uzalishaji wa gesi asilia
Kata taka za majani kwenye vipande vidogo, ongeza maji ili kuviwezesha kuingia ndani ya mfumo kwa urahisi.
Kisha nyenzo huanza kutengana na kuoza, na baadaye gesi ya methane huanza kuzalishwa.
Faida
Gesi asilia husaidia kusafisha mazingira, huokoa umeme na hupunguza gharama zake.