Baada ya kuvuna, ubora wa nyanya hupungua. Utunzaji mzuri wakati wa kuvuna na usafirishaji husababisha mapato bora.
Kupata nyanya bora huanza na jinsi kuvuna au kuchuma kunavyo fanyika. Chuma au vuna asubuhi wakati hali ya hewa ni baridi ili kuepuka kuharibika. Wakati wa kuvuna, chuma kwa uangalifu na uweke nyanya kwenye vikapu. Usitupe nyanya. Hifadhi nyanya kwenye kivuli baada ya kuchuma.
Kusafirisha nyanya
Afadhali tumia kreti za plastiki kwa usafirishaji wa nyanya. Zifunika ikiwa unatumia vikapu ili kuepuka uharibifu. Epuka kurunda nyanya ili kuokoa zile za chini kabisa. Hifadhi nyanya kwenye kivuli, na usivirushe vyombo vya kuhifadhi. Epuka kuweka nyanya moja kwa moja kwa udongo.
Tenganisha na kuchambua nyanya kabla ya kuzisafirisha ili kuondoa zilizoharibika na zilizopasuka. Kisha weka nyanya kwenye kreti au kikapu kwa uangalifu. Safirisha nyanya usiku au asubuhi mapema wakati joto liko chini.
Wakati wa kuvuna
Wakati wa kuvuna hutegemea kama nyanya ni za kuuza katika soko la karibu au la mbali. Kwa soko la karibu, vuna wakati nyanya ni nyekundu. Kwa soko la mbali, changanya nyekundu na zile zinazoanza kugeuka nyekundu.