Wakati wa ukame au kiangaazi, nyasi ni tatizo kubwa linalowakabili wafugaji katika kulisha mifugo yao, na hii hupunguza ubora wa bidhaa za mifugo.
Ujumuishaji wa mbinu kadhaa za ufugaji hufanywa ili kupunguza changamoto zinazokabiliwa na wafugaji. Jamii hujihusisha na mbinu shirikishi kama vile mbinu bora za ufugaji ili kuzalisha malisho (nyasi) ya mifugo.
Ukuzaji wa nyasi
Chagua eneo la ardhi kwa ajili ya kupanda malisho na uandae ardhi vizuri. Wakati wa kuandaa ardhi, kata miti midogo ili uweze kulima udongo kwa urahisi. Lima ardhi, tengeneza mashimo madogo na chimba mifereji ya kutiririsha maji.
Vile vile baada ya hapo, panda mbegu za nyasi (malisho), Weka maji kwenye mifereji na palilia baada ya siku 14. Baada ya siku 21, ongeza maji shambani mara 3 au 4. Vuna nyasi baada ya siku 45 na uzikaushe kwa siku moja au 2 na kisha uzihifadhi kwa mafungu.
Mbinu za kuhifadhi nyasi husaidia kutoa chakula cha mifugo wakati kinapohitajika, na pia huongeza uwezo wa kustahimili ukame.
Kupitia uzalishaji wa nyasi, jamii hukidhi mahitaji yao na pia huongeza kwenye mlo wao kwa lishe bora. Hii huboresha ustawi wa wakulima.