Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha misimu ya mvua isiyotabirika pamoja na mafuriko, ukame ambavyo huathiri utoshelevu wa chakula, na hivyo basi uzalishaji mdogo wa mazao na chakula kutoka mashambani.
Kenya ni nchi inayoweza kuzalisha viazi kutokana na hali ya hewa baridi katika maeneo ya nyanda za juu. Kilimo bora huwasaidia wakulima kukabiliana na changamoto za maji duni wakati wa uzalishaji wa chakula, pamoja na kuwafunza mbinu sahihi za umwagiliaji. Mbinu bora za umwagiliaji ni pamoja na; kutumia kinyunyuziaji, kutumian njia ya matone, na umwagiliaji kwa mikono ingawa umwagiliaji kwa mikono ndio njia duni. Mbinu za kuhifadhi maji ni pamoja na; kuweka matandazo, na kutumia bonde ili kuhifadhi maji ndani ya mmea.
Uzalishaji wa viazi
Uzalishaji mdogo wa viazi husababishwa na wakulima kutumia mbegu duni ambazo huhimiza wadudu na kupunguza mavuno.
Njia maalum ya uzalishaji wa miche kwenye chupa, ambayo hujulikana kama ‘tissue culture’ huruhusu upandaji wa haraka wa mimea mingi yenye sifa sawa, na mimea huzalisha mazao ndani ya miezi minane. Mbinu za kawaida za uzalishaji huchukua takriban miaka minne na nusu kutoa mbegu zilizoidhinishwa.
Hydroponics (ukuzaji wa mmea bila udongo)
Mimea ya ambayo hukuzwa kwa mbinu ya hydroponic huzalisha miche yenye afya bila isiyo na magonjwa yanayoenezwa na udongo. Changanya udongo wa kuotesha miche (coco peat) na pumice, panda vipandikizi kwa umbali wa cm 20.
Coco peat ina uwezo wa kuhifadhi unyevu ambao unaweza kutolea vipandikizi maji. Pumice ni udongo ambao hutoka kwa nyenzo za miamba ya volkeno. Kutoka kwa kipandikizi fulani unaweza kupata kama vipandikizi 15 vidogo. Ni ghali kutakasa udongo wote shambani kwa ajili ya kuua viini.
Soma zaidi juu ya uzalishaji wa miche safi ya viazi kupitia mfumo wa hydroponics sehemu ya 2