Kubadilisha mbegu huongeza hatari ya magonjwa kama vile mnyauko wa bakteria. Mazao kama, canola, Brassica napus ambayo hutoa ulinzi asili kwa viazi, na hivyo kupunguza idadi ya wadudu wavamizi wa mbegu.
Kupanda viazi shambani hili hilo kunapendekezwa mara moja tu katika miaka minne ili kupunguza mashambulizi ya magonjwa na wadudu kwa mbegu safi. Epuka kupanda pilipili, nyanya, katika shamba la viazi, kwani vinaweza kuhimiza uvamizi vimelea vilivyopo kwenye udongo.
Viazi zinaweza kuzungushwa na mazao kama vile; black nightshade, viazi vitamu, malenge, mchicha, n.k.
Mbinu ya uzalishaji wa miche kwenye chupa “Tissue culture”
Muda mwingi huchukuliwa katika uzalishaji wa wa mazao ya mizizi kwa kutumia njia za kawaida. Kusambaza taarifa za kilimo za kisasa huwasaidia wakulima kujua aina bora za kupanda.
Mbinu ya tissue culture hutoa takriban miche 2100 katika mwaka mmoja na nusu ikilinganishwa na njia ya kawaida ambayo hutoa takriban miche 420 kwa miaka minne na nusu.
Ufanisi wa mbinu ya tissue culture ni wa juu sana, na huokoa wakati, nafasi na gharama ya vibarua.
Aeroponics
Aeroponics ni mbinu ya uzalishaji ambapo mimea hukuzwa hewani kuhu myeyusho wa virutubishi ukinyunyiziwa kwenye mizizi yake. Ingawa mbinu hii ni ghali, unaweza kuzuia wadudu na magonjwa ya mazao.
Panda vipandikizi vya mizizi kwenye shimo maalum kwa umbali wa cm 20 ili kuruhusu mizizi kuninginia. Nyunyizia mizizi na myeyusho wa virutubisho na madini.
Kilimo hai
Kilimo hai ni kilimo bila kutumia kemikali na mbolea zisizo za asili. Dawa asili na dondoo za mitishamba hutumiwa kudhibiti wadudu na magonjwa.
Kilimo hai kinaweza kuwa ghali. Inachukua takriban tani 20 za mbolea kwa ekari moja.
Bidhaa za kilimo hai hupunguza maambukizi na magonjwa katika mwili wa binadamu.