»Vidokezo kuhusu Kiasi Gani cha Pesa/Bajeti Unachohitaji Kuanzisha ufugaji wa kuku wa mayai«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=uWhYgoBhMYA

Muda: 

00:10:35
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Africhic

Ili kuanza ufugaji wa kuku 500, iwapo banda lipo tayari, unahitaji gharama ya jumla ya dola 10,937.75. Vifaranga wa siku 500 hugharimu dola 1 kila kimoja.

Sehemu kubwa ya gharama zote ni gharama za pesa za kuanzisha, ambazo hazitahitajika katika ufugaji unaofuata.

Banda la kutunzia vifaranga

Ili kutengeneza eneo la kutunzia vifaranga, unahitaji vipande vitatu vya mbao nyembamba, kila kimoja hugharimu dola 6. Tumia kilo 5 za masanduku ya karatasi kutengeneza sakafu katika wiki mbili za kwanza, kila sunduka likigharimu nusu dola. Ili kuendela kuandaa sakafu ya chumba kikuu na eneo la kutunzia vifaranga hadi kuvitenganisha, tumia ujazo wa gari moja la kanta la pumba ya mbao kwa dola 50.

Kupasha joto kwenye eneo la kutunzia vifaranga kunahitaji mifuko 5 ya briketi au mkaa kwa dola 12 kila moja, na nyungu au jiko 4 kwa dola 15 kila moja.

Malisho

Kifaranga kimoja hula gramu 45 za chakula cha msingi kwa siku. Kwa muda wa siku 60 vifaranga 500 watakula kilo 22.5 kwa gharama ya dola 702.

Kuku wachanga 500 hula mifuko 36 ya chakula, ambacho hugharimu dola 761. Chakula cha kuku wa mayai hulishwa kwa kuku hadi kukoma hedhi ambayo ni katika wiki ya 72 au siku ya 504. Mifuko 384 inayolishwa kuku 500 inagharimu dola 8,824. Gharama za mirija ya kulisha 25 ni dola 5.6 kila mrija. Vyombo 10 vya kunyeshea maji hugharimu dola 3.5 kila kimoja.

Vitamini na dawa za kuua viini

Gharama ya jumla ya chanjo ni dola 26.7 ambazo ni pamoja na kideri au mdondo, ndui na gumboro.

Kwa vitamini, Kilo 5 za vitamini ya kuanzia hugharimu dola 8.05 kila kilo moja. Tumia dawa ya Alamyein ya 100ml kwa gharama ya dola 3.3 kila ml kwa ajili ya kutibu vidonda vinavyosababishwa hasa na kujikula.

Lita 5 za dawa ya minyoo hugharimu dola 8 kila lita. Wakati wa kutumia dawa hii yeyusha 50 ml ya dawa katika lita 20 za maji. Kwa udhibiti wa maambukizi ya matumbo tumia 5kg ya Alicerlyle ambayo hugharimu dola 75.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:53Gharama ya kuanzisha ufugaji wa kuku.
00:5401:33Ili kutengeneza eneo la kutunzia vifaranga, unahitaji vipande vitatu vya mbao nyembamba, kilo 5 za masanduku ya karatasi, na pumba ya mbao.
01:3302:03Kupasha joto kwenye eneo la kutunzia vifaranga kunahitaji mifuko 5 ya briketi au mkaa
02:0402:58Vifaranga 500 watakula kilo 22.5 kwa gharama ya dola 702
02:5903:49Growers mash is fed to chicken up to POL which is approximately day 120.
03:5004:20Kuku wachanga 500 hula mifuko 36 ya chakula, ambacho hugharimu dola 761.
04:2105:09Kuku moja hula gramu 90 ya chakula cha kuku wa mayai mwanzoni mwakutaga, na gramu 105 katika kiwango cha juu cha kutaga.
05:1005:48Chakula cha kuku wa mayai hulishwa kwa kuku hadi kukoma hedhi ambayo ni katika wiki ya 72 au siku ya 504.
05:4906:30Gharama ya jumla ya mifuko 374.4 ya chakula cha kuku wa mayai kwa siku 384 ni dola 8,424.
06:3107:17Gharama ya jumla ya chanjo ni dola 26.7
07:1807:53Kilo 5 za vitamini ya kuanzia hugharimu dola 8.05 kila kilo moja. Dawa ya Alamyein ya 100ml kwa gharama ya dola 3.3 kila ml.
07:5408:27Lita 5 za dawa ya minyoo hugharimu dola 8 kila lita. 5kg ya Alicerlylehugharimu dola 75.
08:2809:15Gharama za mirija ya kulisha 25 ni dola 5.6 kila mrija. Vyombo 10 vya kunyeshea maji hugharimu dola 3.5 kila kimoja
09:1610:35Gharama ya uzalishaji kwa ujumla ni dola 10,937.75.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *