Tasnia ya kuku inakua kwa kasi, lakini inakabiliwa na changamoto kadhaa.
Gharama kubwa ya chakula ni mojawapo ya changamoto zinazokabili tasnia ya kuku, na hivyo mtu anatakiwa kuwa na uwezo wa kupata zaidi kutokana na rasilimali chache zilizopo. Wafugaji hufuga kuku wa nyama kwa muda mfupi, yaani kati ya siku 32 hadi 6o. Hivyo basi, mzunguko mzima wa uzalishaji wa kuku huchukua kati ya wiki 4 hadi 8.
Maandalizi ya ufugaji wa kuku wa nyama
Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku wa nyama, unapaswa kujiandaa kimwili, kihisia na kifedha yaani banda linapaswa kujengwa na pia kusafishwa na kunyunyiziwa dawa za kuua viini mara kwa mara. Pia hakikisha kwamba kuna vihori vya chakula na vya maji, pamoja ma mahali pa kutunzia vifaranga.
Kihisia, inabidi uwe umejiandaa kwa sababu usipojiandaa basi utalemewa na changamoto ya kushughulikia vifaranga kwa saa 24 kila siku.
Kifedha, hakikisha kuwa una fedha zote zinazotosha kununua malisho, dawa na chanjo. Fuga idadi ya kuku ambayo unaweza kushughulikia kifedha.
Hifadhi ndani ya orodha yako namabari za wataalam kama madaktari wa mifugo ambao unaweza kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwao.
Anza kwa kufanya utafiti wa soko na ufuge tu idadi ya kuku ambayo itapata soko tayari ili kuepuka kupata hasara.