Vipanda bora vya mihogo husababisha mavuno mengi. Kutumia tena vipanda husambaza magonjwa kama ugonjwa wa mistari ya kahawia na batobato inayosababishwa na virusi.
Kuzalisha vipanda bora vya muhogo kunahitaji hatua fulani, na hivyo kusababisha mazao mazuri. Vipanda vya mihogo haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu. Wakulima hukuza mihogo lakini ni wachache wanaonunua vipanda.
Vipanda bora vya muhogo
Anza kwa kuchagua eneo linalofaa na kuandaa shamba mapema ili kufaidika na mvua ya mapema, na kuhakikisha udongo una rutuba ili kuwezesha mimea kustawi.
Amua aina za kutumia na kuvishughulikia vipanda inavyotakiwa ili kufanikiwa na mapato ya juu. Pia, chagua eneo lisilo na ugonjwa wa mihogo, na tumia vipanda bora vilivyothibitishwa ili kuepuka kushindwa kuzalisha.
Kwa kuongezea, kuza mihogo kwenye udongo ulio na rutuba pamoja na kiasi kidogo cha changarawe,kwa sababu ya uwezo wake wa kuhifadhi maji, na ni rahisi kufanyika kazi. Lima shamba lako mapema ili uweze kupanda mara tu mvua inaponyesha.
Tumia vipanda vyenye afya vinavyostahimili magonjwa kutoka kwa shirika la utafiti, ama muuzaji aliyeidhinishwa.
Njia ya kupanda
Tumia (mashina) vipanda vilivyo komaa, ambavyo vilidumu wakati wa miezi 9–12, na havina ugonjwa wowote, ili kuwezesha kuota vizuri na kutoa mazao mengi. Vipanda hivi vinafaa kuwa vifupi, na hakikisha kwamba unavipanda mara ili kuviwezesha kuota vizuri na mimea iwe na nguvu.
Nunua mashina kamili ambazo zinakaguliwa ili kuhakikisha ukuaji mzuri. Epuka kuchukua au kusafirisha vipanda wakati wa jua kali ili kudhibiti upungufu wa maji yaliyomu. Kuwa mwangalifu unapopakia na kupakua vipanda ili usivikwaruze.
Katakata mashina katika vipande vya sentimita 20–30 na hakikisha kila kipande kiwe na nundu 5 ili kiweze kuota . Hifadhi vipanda chini ya kivuli, huku ukivimwagilia maji ili kudhibiti kukauka kwa mashina. Mwishowe panda katika nafasi ya mita 1 kwa mita 1 ili kupata kiwango cha juu cha uzalishaji