»Vipanda bora vya muhogo«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/quality-cassava-planting-material

Muda: 

00:15:40
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Vipanda bora vya mihogo husababisha mavuno mengi. Kutumia tena vipanda husambaza magonjwa kama ugonjwa wa mistari ya kahawia na batobato inayosababishwa na virusi.

Kuzalisha vipanda bora vya muhogo kunahitaji hatua fulani, na hivyo kusababisha mazao mazuri. Vipanda vya mihogo haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu. Wakulima hukuza mihogo lakini ni wachache wanaonunua vipanda.

Vipanda bora vya muhogo

Anza kwa kuchagua eneo linalofaa na kuandaa shamba mapema ili kufaidika na mvua ya mapema, na kuhakikisha udongo una rutuba ili kuwezesha mimea kustawi.

Amua aina za kutumia na kuvishughulikia vipanda inavyotakiwa ili kufanikiwa na mapato ya juu. Pia, chagua eneo lisilo na ugonjwa wa mihogo, na tumia vipanda bora vilivyothibitishwa ili kuepuka kushindwa kuzalisha.

Kwa kuongezea, kuza mihogo kwenye udongo ulio na rutuba pamoja na kiasi kidogo cha changarawe,kwa sababu ya uwezo wake wa kuhifadhi maji, na ni rahisi kufanyika kazi. Lima shamba lako mapema ili uweze kupanda mara tu mvua inaponyesha.

Tumia vipanda vyenye afya vinavyostahimili magonjwa kutoka kwa shirika la utafiti, ama muuzaji aliyeidhinishwa.

Njia ya kupanda

Tumia (mashina) vipanda vilivyo komaa, ambavyo vilidumu wakati wa miezi 9–12, na havina ugonjwa wowote, ili kuwezesha kuota vizuri na kutoa mazao mengi. Vipanda hivi vinafaa kuwa vifupi, na hakikisha kwamba unavipanda mara ili kuviwezesha kuota vizuri na mimea iwe na nguvu.

Nunua mashina kamili ambazo zinakaguliwa ili kuhakikisha ukuaji mzuri. Epuka kuchukua au kusafirisha vipanda wakati wa jua kali ili kudhibiti upungufu wa maji yaliyomu. Kuwa mwangalifu unapopakia na kupakua vipanda ili usivikwaruze.

Katakata mashina katika vipande vya sentimita 20–30 na hakikisha kila kipande kiwe na nundu 5 ili kiweze kuota . Hifadhi vipanda chini ya kivuli, huku ukivimwagilia maji ili kudhibiti kukauka kwa mashina. Mwishowe panda katika nafasi ya mita 1 kwa mita 1 ili kupata kiwango cha juu cha uzalishaji

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:39Wakulima hukuza mihogo, lakini ni wachache wanaonunua vipanda.
00:4001:12Kutumia tena vipanda husambaza magonjwa
01:1302:44Vipanda bora vya mihogo husababisha mavuno mengi
02:4503:55Mashina ya muhogo yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
03:5604:04Jinsi ya kuzalisha vipanda bora vya muhogo.
04:0504:09Chagua eneo linalofaa na pia andaa shamba mapema
04:1004:14Hakikisha udongo una rutuba
04:1504:21Amua aina za kutumia na kuvishughulikia
04:2204:41Chagua eneo lisilo na ugonjwa wa mihogo
04:4205:16Tumia vipanda bora vilivyothibitishwa
05:1705:43Kuza mihogo kwenye udongo ulio na rutuba pamoja na kiasi kidogo cha changarawe
05:4406:33Lima shamba lako mapema
06:3407:33Tumia vipanda vyenye afya vinavyostahimili magonjwa
07:3407:40Jinsi ya kuzalisha zao bora
07:4107:57Tumia (mashina) vipanda vilivyo komaa, ambavyo vilidumu wakati wa miezi 9–12,
07:5808:31Kamwe, usitumie vipanda kutoka kwa mashamba yaliyovamiwa na magonjwa.
08:3209:04Vipanda hivi vinafaa kuwa vifupi, na hakikisha kwamba unavipanda mara
09:0509:44Nunua mashina kamili ambazo zinakaguliwa kabla ya msimu wa mvua
09:4509:50Epuka kuchukua au kusafirisha vipanda wakati wa jua kali
09:5110:01Kuwa mwangalifu unapopakia na kupakua vipanda
10:0211:02Hifadhi vipanda chini ya kivuli, huku ukivimwagilia maji mara kwa mara,
11:0311:44Katakata mashina katika vipande vya sentimita 20–30 na hakikisha kila kipande kiwe na nundu 5
11:4512:00Chomeka unusu wa vipanda kweneye udongo, na nudu zilielekea juu.
12:0112:24Tumia vipanda virefu katika msimu wa kiangazi
12:2512:57Panda katika nafasi ya mita 1 kwa mita 1
12:5815:40Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *