Mchicha ni mmea wa kila mwaka na hukua hadi urefu wa 30 cm. Unaweza kupandwa katika aina zote za udongo, hata hivyo udongo wa tifutifu ambao una alkali kidogo ni bora.
Mchicha unaweza kushambuliwa na wadudu kadhaa kama vile mbawakau na vidukari. Magonjwa ni pamoja na; ubwiri, mnyauko, uoza wa mizizi na ukungu, lakini kwa njia sahihi haya yanaweza kudhibitiwa kwa urahisi.
Mchicha hustawi vizuri kwenye joto la nyuzi joto 15 – 20 celsius lakini pia hustahimili kiwango cha chini cha nyuzijoto 10, na kisichozidi nyuzi joto 30.
Hatua za kilimo
Anza kwa kulima udongo ili kulainika, ongeza samadi na kilo 25 za nitrojeni kwa hekta ili kuongeza rutuba ya udongo. Pili, loweka mbegu kwenye maji usikukucha kabla ya kupanda ili kuboresha uotaji.
Pia panda mbegu kwa kutawanya au kwa safu katika miezi inayofaa kwa mikoa tofauti. Daima weka mbolea ili kutimiza mahitaji ya virutubisho vya mimea, na kuongeza mavuno.
Dhibiti magugu mara 2 – 3 ili kupunguza ushindani wa virutubisho na kulainisha udongo kwa ajili ya uingizaji mzuri wa hewa. Daima nyunyiza viuatilifu maalum, na viuakuvu. Panda aina sugu ili kudhibiti wadudu na magonjwa ya mchicha. Hatimaye, Vuna aada ya siku 35 – 40 kwa kukata majani ya nje ili kuruhusu ukuaji zaidi wa majani.