»Kilimo – Maisha ya Mchicha«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=JNEgbypt0Js&t=365s

Muda: 

00:08:37
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Tutorials Point (India) Ltd.

Mchicha ni mmea wa kila mwaka na hukua hadi urefu wa 30 cm. Unaweza kupandwa katika aina zote za udongo, hata hivyo udongo wa tifutifu ambao una alkali kidogo ni bora.

Mchicha unaweza kushambuliwa na wadudu kadhaa kama vile mbawakau na vidukari. Magonjwa ni pamoja na; ubwiri, mnyauko, uoza wa mizizi na ukungu, lakini kwa njia sahihi haya yanaweza kudhibitiwa kwa urahisi.

Mchicha hustawi vizuri kwenye joto la nyuzi joto 15 – 20 celsius lakini pia hustahimili kiwango cha chini cha nyuzijoto 10, na kisichozidi nyuzi joto 30.

Hatua za kilimo

Anza kwa kulima udongo ili kulainika, ongeza samadi na kilo 25 za nitrojeni kwa hekta ili kuongeza rutuba ya udongo. Pili, loweka mbegu kwenye maji usikukucha kabla ya kupanda ili kuboresha uotaji.

Pia panda mbegu kwa kutawanya au kwa safu katika miezi inayofaa kwa mikoa tofauti. Daima weka mbolea ili kutimiza mahitaji ya virutubisho vya mimea, na kuongeza mavuno.

Dhibiti magugu mara 2 – 3 ili kupunguza ushindani wa virutubisho na kulainisha udongo kwa ajili ya uingizaji mzuri wa hewa. Daima nyunyiza viuatilifu maalum, na viuakuvu. Panda aina sugu ili kudhibiti wadudu na magonjwa ya mchicha. Hatimaye, Vuna aada ya siku 35 – 40 kwa kukata majani ya nje ili kuruhusu ukuaji zaidi wa majani.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:04Mchicha ni mmea wa kila mwaka na hukua hadi urefu wa 30 cm
01:1800:00Mchicha hustahimili hali ya kibaridi na joto. Joto la juu husababisha hasara.
01:3101:47Mchicha hustawi vizuri kwenye joto la nyuzi joto 15 – 20 celsius
01:4802:10Hatua za kilimo cha mchicha.
02:1103:07Lima udongo mara 4 hadi 6, ongeza mabaki ya shambani na kilo 25 za nitrojeni kwa hekta.
03:0803:18Tengeneza vitalu na mifereji ya umwagiliaji.
03:1903:57Loweka mbegu kwenye maji. Panda mbegu kwa kutawanya
03:5804:57Mwagilia shamba lote baada ya kupanda na wakati mazao yanapotokea.
04:5805:35Weka mbolea shambani na udhibiti magugu mara 2–3.
05:3606:49Nyunyizia dawa maalum za kuua wadudu, viuatilifu na upande aina sugu.
06:5007:57Vuna aada ya siku 35 – 40 kwa kukata majani ya nje.
07:5808:37Osha majani, ainisha kabla ya kuuza sokoni.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *