»Ufugaji wa nguruwe sehemu ya pili«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=cK-fDILDuAA

Muda: 

00:08:09
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

royaldreamtv

Ufugaji wa nguruwe ni biashara yenye faida kubwa ikiwa usimamizi ufaao na hatua zote za kudhibiti magonjwa zitatekelezwa kwa usahihi.

Wakati wa kuanzisha ufugaji hakikisha kuwa malisho yanayotolewa kwa wanyama yana virutubisho vyote vinavyohitajika. Malisho ni pamoja na; ugali, mahindi, mihogo, maganda ya mihogo, unga wa muhogo, makapi ya mpunga na nafaka. Hata hivyo unaweza kupanda baadhi ya mazao kwa ajili ya kutengeneza malisho ili kupunguza gharama za ufugaji. Pia zingatia kupanua uzalishaji ili kupata kipato zaidi.

Hatua za usimamizi

Daima tengeneza banda linalofaa ili kuhimiza mzunguko wa hewa. Tengeneze viumbe vidogo vya kiasili (IMO) ambavyo huzuia harufu mbaya na nzi kutoka kwenye banda la nguruwe. Pia unapaswa kushauriana na wataalam wa nguruwe ili kupata maarifa ya kimsingi kwa mfano; habari juu ya aina, gharama ya malisho, utengenezaji wa malisho, dawa, na mbinu bora za kuongeza faida.

Tengeneza mkakati wako wa uuzaji, mpango wa uuzaji ili kuuza nguruwe kwa uzani wa soko unaohitajika.

Jenga banda kwa kila aina ya nguruwe ili kurahisisha usimamizi sahihi wa mifugo. Pia epuka kuzaliana kati ya nguruwe wa jamii hiyo hiyo. Tafuta aina bora za nguruwe ambazo zina sifa unazotaka. Lisha nguruwe kwa lishe bora ambalo hutoa virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji wa haraka.

Pia tumia mchanganyiko sahihi wa malisho ili kupunguza gharama, kwa kushauriana na wataalam wa nguruwe na kufanya utafiti. Vile vile, dumisha usafi wa mazingira kwa kutumia hatua zifaazo kuzuia magonjwa, na hivyo kupunguza gharama za madawa.

Jenga mifereji mizuri ambayo hutiririsha kinyesi na mkojo wa nguruwe kwa urahisi. Tumia mfumo wa kuweka matandazo bandani, ambao husaidia nguruwe kuwa na afya njema. Ni muhimu kuwafunza wafanyikazi, pamoja na kushauriana na daktari wa mifugo ili kufanikiwa na ufugaji wa nguruwe.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:40Tengeneza banda bora, viumbe vidogo vya kiasili.
01:4102:21Shauriana na wataalam wa nguruwe ili kupata maarifa. Tengeneza mkakati wako wa uuzaji.
02:2203:18Jenga banda kwa kila aina ya nguruwe
03:1904:26Pia epuka kuzaliana kati ya nguruwe wa jamii hiyo hiyo. Tafuta aina bora za nguruwe ambazo zina sifa unazotaka.
04:2704:56Lisha nguruwe kwa lishe bora
04:5705:25Tumia mchanganyo sahihi wa malisho, panda baadhi ya mazao kwa ajili ya kutengeneza malisho.
05:2606:44Dumisha usafi wa mazingira kwa kutumia hatua zifaazo kuzuia magonjwa.
06:4506:55Jenga mifereji mizuri ambayo hutiririsha kinyesi na mkojo. Tumia mfumo wa kuweka matandazo bandani.
06:5607:45Wafunze wafanyikazi, pamoja na kushauriana na daktari wa mifugo.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *