Ufugaji wa nguruwe ni biashara yenye faida kubwa ikiwa usimamizi ufaao na hatua zote za kudhibiti magonjwa zitatekelezwa kwa usahihi.
Wakati wa kuanzisha ufugaji hakikisha kuwa malisho yanayotolewa kwa wanyama yana virutubisho vyote vinavyohitajika. Malisho ni pamoja na; ugali, mahindi, mihogo, maganda ya mihogo, unga wa muhogo, makapi ya mpunga na nafaka. Hata hivyo unaweza kupanda baadhi ya mazao kwa ajili ya kutengeneza malisho ili kupunguza gharama za ufugaji. Pia zingatia kupanua uzalishaji ili kupata kipato zaidi.
Hatua za usimamizi
Daima tengeneza banda linalofaa ili kuhimiza mzunguko wa hewa. Tengeneze viumbe vidogo vya kiasili (IMO) ambavyo huzuia harufu mbaya na nzi kutoka kwenye banda la nguruwe. Pia unapaswa kushauriana na wataalam wa nguruwe ili kupata maarifa ya kimsingi kwa mfano; habari juu ya aina, gharama ya malisho, utengenezaji wa malisho, dawa, na mbinu bora za kuongeza faida.
Tengeneza mkakati wako wa uuzaji, mpango wa uuzaji ili kuuza nguruwe kwa uzani wa soko unaohitajika.
Jenga banda kwa kila aina ya nguruwe ili kurahisisha usimamizi sahihi wa mifugo. Pia epuka kuzaliana kati ya nguruwe wa jamii hiyo hiyo. Tafuta aina bora za nguruwe ambazo zina sifa unazotaka. Lisha nguruwe kwa lishe bora ambalo hutoa virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji wa haraka.
Pia tumia mchanganyiko sahihi wa malisho ili kupunguza gharama, kwa kushauriana na wataalam wa nguruwe na kufanya utafiti. Vile vile, dumisha usafi wa mazingira kwa kutumia hatua zifaazo kuzuia magonjwa, na hivyo kupunguza gharama za madawa.
Jenga mifereji mizuri ambayo hutiririsha kinyesi na mkojo wa nguruwe kwa urahisi. Tumia mfumo wa kuweka matandazo bandani, ambao husaidia nguruwe kuwa na afya njema. Ni muhimu kuwafunza wafanyikazi, pamoja na kushauriana na daktari wa mifugo ili kufanikiwa na ufugaji wa nguruwe.