Matango ni matunda yenye afya, ambayo hulimwa kwa matumizi ya nyumbani na kuongeza kipato kwa wakulima. Matango yanaweza kukuzwa kwa urahisi nyumbani na huhitaji nafasi ndogo.
Unapopanda matango, tengeneza mashimo chini ya kikombe ambacho kitakachotumika kukuza mmea, hii husaidia kuondoa maji ya ziada. Tumia udongo wa kichanga kwa kupanda mbegu kwani kichanga huondoa maji ya ziada na hivyo kustawisha mmea na ukuaji wa mizizi.
Kupanda hadi kuvuna
Loweka mbegu kwenye maji kwa muda wa saa 2 ili unyevu upenyeze ndani ya mbegu. Kisha funika mbegu kwa karatasi na uziweke kwenye chombo. Nyunyizia maji kwenye karatasi iliyo na mbegu na uziweka ndani ya chombo. Kisha funga chombo ili kuhifadhi unyevu ndani.
Acha mbegu ndani ya chombo kwa muda wa saa 12 ili zioteshe mizizi na uzipande kwenye vikombe vyenye mashimo chini. Changanya udongo na pumba za mpunga na samadi ya ng‘ombe ili kuongeza rutuba ya udongo. Kisha pandikiza miche baada ya siku 7.
Pia funika udongo na karatasi ya nailoni baada ya kupandikiza ili kuhifadhi unyevu kwenye udongo na kuzuia ukuaji wa magugu. Simika fito ambao zitasaidia kuthibitisha mimea kwa ukuaji mzuri. Mwishowe, chavusha maua kwa mikono ili kusaidia katika uundaji wa matunda zaidi kwa ongezeko la mavuno.