»Kupanda matango nyumbani«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=0uBuHOo5VO8

Muda: 

00:06:06
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Garden Yard

Matango ni matunda yenye afya, ambayo hulimwa kwa matumizi ya nyumbani na kuongeza kipato kwa wakulima. Matango yanaweza kukuzwa kwa urahisi nyumbani na huhitaji nafasi ndogo.

Unapopanda matango, tengeneza mashimo chini ya kikombe ambacho kitakachotumika kukuza mmea, hii husaidia kuondoa maji ya ziada. Tumia udongo wa kichanga kwa kupanda mbegu kwani kichanga huondoa maji ya ziada na hivyo kustawisha mmea na ukuaji wa mizizi.

Kupanda hadi kuvuna

Loweka mbegu kwenye maji kwa muda wa saa 2 ili unyevu upenyeze ndani ya mbegu. Kisha funika mbegu kwa karatasi na uziweke kwenye chombo. Nyunyizia maji kwenye karatasi iliyo na mbegu na uziweka ndani ya chombo. Kisha funga chombo ili kuhifadhi unyevu ndani.

Acha mbegu ndani ya chombo kwa muda wa saa 12 ili zioteshe mizizi na uzipande kwenye vikombe vyenye mashimo chini. Changanya udongo na pumba za mpunga na samadi ya ng‘ombe ili kuongeza rutuba ya udongo. Kisha pandikiza miche baada ya siku 7.

Pia funika udongo na karatasi ya nailoni baada ya kupandikiza ili kuhifadhi unyevu kwenye udongo na kuzuia ukuaji wa magugu. Simika fito ambao zitasaidia kuthibitisha mimea kwa ukuaji mzuri. Mwishowe, chavusha maua kwa mikono ili kusaidia katika uundaji wa matunda zaidi kwa ongezeko la mavuno.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:25Hatua za kukua na kupanda matango.
00:2600:34Loweka mbegu kwenye maji kwa masaa 2.
00:3500:43Funika mbegu kwenye karatasi na uziweke kwenye chombo
00:4400:50Nyunyizia maji kwenye karatasi iliyo na mbegu na kuziweka kwenye chombo. Kisha funga chombo
00:5101:07Acha mbegu ndani ya chombo kwa muda wa saa 12 ili zioteshe mizizi na uzipande kwenye vikombe vyenye mashimo chini.
01:0802:17Tumia udongo wa kichanga kwa kupanda miche.
02:1803:06Changanya udongo na pumba za mpunga na samadi ya ng‘ombe. Kisha pandikiza miche.
03:0704:14Funika udongo na karatasi ya nailoni. Simika fito ambao zitasaidia kuthibitisha mime.
04:1505:54Chavusha maua kwa mikono, vuna bada ya siku 90.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *