»Kilimo cha soya«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=oUcstNH0z54

Muda: 

00:05:54
Imetengenezwa ndani: 
2010

Imetayarishwa na: 

obedkofi1

Ili kuongeza mavuno ya soya, mbinu sahihi za usimamizi lazima zifuatwe wakati wa ukuzaji.

Iwapo utatekeleza kilimo hifadhi , tengeneza shamba lako kwa kufyeka na kuchoma nyasi. Kisha nyunyizia eneo hilo dawa za kuua magugu. Hata hivyo, unaweza pia kulima ardhi ili kulainisha udongo inavyopendekezwa. Nunua mbegu za upanzi za aina bora kutoka kwa kampuni inayoaminika.

Kupanda na kushughulikia soya

Panda soya kwa muachano wa sm 5 hadi 10 ndani ya safu na 60 kati ya safu. Panda soya baada ya mvua, kwenye mashimo yenye kina cha 2cm na kisha mbegu hufunikwa na udongo kidogo.

Udhibiti wa magugu ni muhimu katika kilimo cha soya. Kipindi muhimu zaidi cha kupalilia ni kati ya siku ya 15 hadi 25 baada ya kupanda, lakini ni muhimu kung’oa magugu shambani kutoka hatua ya kupanda hadi kuvuna. Magugu yanaweza kudhibitiwa kwa mikono au kwa kutumia dawa zinazopendekezwa.

Vuna soya wakati majani ni rangi ya manjano, na yatandaze mavuno ili yakauke. Baada ya kukausha, pura ili kupata nafaka bora ya soya.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:54Iwapo utatekeleza kilimo hifadhi , tengeneza shamba lako kwa kufyeka na kuchoma nyasi.
00:5501:00Kisha nyunyizia eneo hilo dawa za kuua magugu.
01:0101:12Hata hivyo, unaweza pia kulima ardhi ili kulainisha udongo inavyopendekezwa
01:1301:35Panda soya kwa muachano wa sm 5 hadi 10 ndani ya safu na 60 kati ya safu
01:3602:04Nunua mbegu kutoka kwa kampuni ya mbegu inayoaminika. Panda soya kwenye mashimo yenye kina cha 2cm.
02:0502:32Ng’oa magugu shambani kutoka kupanda hadi kuvuna.
02:3302:44Magugu yanaweza kudhibitiwa kwa mikono au kwa kutumia dawa zinazopendekezwa.
02:4503:16Vuna soya wakati majani ni rangi manjano, na yatandaze mavuno ili yakauke.
03:1703:54Credits

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *