Ili kuongeza mavuno ya soya, mbinu sahihi za usimamizi lazima zifuatwe wakati wa ukuzaji.
Iwapo utatekeleza kilimo hifadhi , tengeneza shamba lako kwa kufyeka na kuchoma nyasi. Kisha nyunyizia eneo hilo dawa za kuua magugu. Hata hivyo, unaweza pia kulima ardhi ili kulainisha udongo inavyopendekezwa. Nunua mbegu za upanzi za aina bora kutoka kwa kampuni inayoaminika.
Kupanda na kushughulikia soya
Panda soya kwa muachano wa sm 5 hadi 10 ndani ya safu na 60 kati ya safu. Panda soya baada ya mvua, kwenye mashimo yenye kina cha 2cm na kisha mbegu hufunikwa na udongo kidogo.
Udhibiti wa magugu ni muhimu katika kilimo cha soya. Kipindi muhimu zaidi cha kupalilia ni kati ya siku ya 15 hadi 25 baada ya kupanda, lakini ni muhimu kung’oa magugu shambani kutoka hatua ya kupanda hadi kuvuna. Magugu yanaweza kudhibitiwa kwa mikono au kwa kutumia dawa zinazopendekezwa.
Vuna soya wakati majani ni rangi ya manjano, na yatandaze mavuno ili yakauke. Baada ya kukausha, pura ili kupata nafaka bora ya soya.