Upunguzaji wa miti ni mchakato wa kuchagua na kuondoa miti msituni.
Upunguzaji wa miti ni
muhimu katika usimamizi wa misitu. Hata hivyo, ni muhimu kujua kwa nini kitendo hicho hufanywa
na mambo yanayoathiri uchaguzi wa miti itakayokatwa. Wakati msitu wako hauna
mimea mingine ardhini, inashauriwa upunguze miti kwaani huku kunamaanisha kuwa matawi ni
manene sana na hayaruhusi mwanga wa jua kupenya.
Wakati sahihi wa kupunguza miti
IIkiwa kuna miti ambayo ina mashina
madogo na matawi machache, inashauriwa uikate.
Unaweza pia kutembea kwenye msitu wako huku ukipima vipenyo vya mashina ili
kujua iwapo msitu wako ni mnene. Vipimo hivyo vinaweza kulinganishwa na vipimo
maalum vilivyotolewa katika machapisho ya ugani wa misitu.
Miti inaweza kukuzwa kati ya
miaka 10 hadi 15 na kisha yote hukatwa
mara moja, au ukaguzi wa mara kwa mara unaweza kufanywa ili kuondoa miti
iliyoharibika na isiyoweza kuuzwa.
Kanuni ya jumla wakati unapunguza
miti ni kwamba uondoe miti nyembamba na kuacha miti mikubwa kwa sababu miti
mikubwa huchukuliwa kuwa na afya zaidi kuliko miti nyembamba.
Umuhimu wa kupunguza miti
Kupunguza miti hutoa nafasi ya
kutosha na virutubishi ambavyo husababisha ukuaji bora wa miti iliyobaki.
Huongeza upenyaji wa mwanga wa
jua ambao huhimiza ukuaji wa mimea zaidi ardhini mwa msitu, na hivyo
kuongeza anuai kadhaa za mfumo ikolojia.
Kupunguza miti huunda msitu wenye afya na kuboresha makazi ya
wanyamapori.