Wakulima ambao hulima mseto wa migomba na kahawa hupata uzalishaji mkubwa na kipato zaidi kuliko wale ambao hawalimi mseto.
Hata hivyo, ili kupata faida kubwa wakulima wanapaswa kuzingatia kanuni za usimamizi zinazofaa, kama vile kupogoa mara kwa mara, kudumisha msongamano unaohitajika, kupunguza idadi ya mimea, na kupogoa.
Faida za kilimo mseto
Huongeza kipato Kwa wakulima.
Huongeza uwepo wa chakula kwa sababu ndizi huvunwa mwaka mzima.
Husababisha uingiaji wa fedha endelevu, na hivyo kusaidia wakulima kukidhi gharama za mahitaji ya kila siku.
Hutoa ongezeko la fedha kwa msimu kwa wakulima, kwani kahawa huvunwa mara mbili.
Huongeza mapato maradufu, kwa sababu ya ongezeko kwa uzalishaji kwenye kipande hicho cha ardhi.
Migomba hutoa kivuli na matandazo kwa mikahawa ambavyo hudhibiti magugu, huhifadhi unyevu wa udongo, hupunguza mmomonyoko wa udongo na huongeza mboji kwenye udongo.