Azolla ni mmea wa kuvu wa majini ambao hupandwa kwenye maji yaliyotuama au bwawa. Ni nzuri kwa wafugaji wa samaki, kuku na ng‘ombe.
Azolla ina protini nyingi, vitamini A, B na C na madini. Upandaji wa azolla huhitaji pembejeo kidogo. Unahitaji tu bwawa, mbolea ya kikaboni na miche ya azolla. Kujenga bwawa kunagharimu takribani Ksh 4000.
Uzalishaji wa Azolla
Chukua mimea ya azolla iliyokomaa kwenye bwawa jipya lenye samadi ndani yake. Tandaza azolla kwenye bwawa. Iache kwa siku 14 ili iweze kukomaa. Azolla huvunwa kila wiki. Unaweza kuvuna kilo 10–15 kwa wiki. Kilo moja huuzwa Ksh 50.
Kila baada ya wiki mbili ongeza mbolea ya kikaboni ambayo itakaa karibu miezi minane.
Safisha bwawa. Baada ya kusafisha bwawa ongeza azolla nyingine.
Faida za Azolla
Huboresha tija kwa wanyama. Azolla hutengenezwa nyumbani na huhitaji matunzo kidogo.
Unaweza kuanzisha kilimo cha azolla kwenye kipande kidogo cha ardhi.
Changamoto
Changamoto za kilimo cha azolla ni wadudu, vyura, viluwiluwi ambavyo kuingia kwenye bwawa. Ili kudhibiti haya, weka uzio kuzunguka bwawa.