Nyanya ni mojawapo ya viungo vinavyotumika sana kupikia katika kila nyumba barani Afrika.
Mahitaji ya nyanya yanazidi kuongezeka. Kabla ya kuanza biashara ya kilimo cha nyanya, amua ukubwa wa uzalishaji, msimu wa kuzalishia na lengo la soko. Ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa nyanya inapaswa kuwa na uingizaji wa hewa bora na bila sumu. Ndiyo maana matumizi ya mbolea za kikaboni yanahitajika. Nyanya zinaweza kustawi katika aina mbalimbali za udongo, lakini udongo wa kichanga ndio bora zaidi, na hustawi vyema katika udongo wenye pH kati ya 5 hadi 6.5.
Vifaa na pembejeo
Mashine na vifaa vinavyohitajika hutegemea ukubwa wa uzalishaji. Unahitaji vifaa/mashine kwa ajili ya kutayarisha ardhi, vinyunyizio, na vifaa vya umwagiliaji.
Pembejeo za nyanya ni pamoja na mbegu za nyanya. Nyanya zimeainishwa kama determinate, semi determinate au indeterminate. Mambo yanayoathiri uchaguzi wa mbegu ni upatikanaji wa mbegu, kiwango wa mavuno, upinzani dhidi ya magonjwa na soko linalokusudiwa. Hakikisha unanunua mbegu kutoka kwa wauzaji walioidhinishwa.
Mbolea huhitajika ili kuongeza rutuba ya udongo na kuhakikisha ukuaji bora wa nyanya. Nyanya huhitaji madini ya nitrojeni, Fosforasi na Potasiamu ambayo hutolewa kupitia mbolea na samadi.
Dawa za magugu huhitajika kwa udhibiti wa magugu.
Kibarua na uuzaji
Unahitaji kuajiri wafanyikazi wa muda inavyohitajika. Shughuli zinazohitaji vibarua ni pamoja na kupanda mbegu, kupandikiza, kuweka mbolea, kulima, kuvuna na nyinginezo.
Kuna soko kubwa la nyanya kwani wanunuzi wa nyanya ni pamoja na watu binafsi, wahudumu wa chakula, migahawa, wasindikaji wa vyakula, maduka makubwa na soko la taifa la mazao.