Baada ya kukamua ng’ombe kwa kutumia mashine tumbukiza kifaa cha kukamulia kwenye ndoo iliyo na dawa ya mastrite, ambayo hufanya kama iodini. Kabla ya kupaka dawa kwenye matiti ya ng’ombe hakikisha kwamba hatakurushia mateke, na kisha chovya matiti kwenye kikombe kilicho na dawa.
Bonyeza kikombe sehemu ya chini ili kupandisha dawa juu na utumbukize matiti kwenye dawa.
Usimamizi wa ndama
Usimamizi wa ndama huanza kabla ya hawajazaliwa hadi kuachishwa kunyonya.
Mafunzo ya usimamizi wa ndama yanapaswa kutolewa kwa wafugaji ili kupunguza athari mbaya za uzazi, na ndama kuzaliwa wamekufa.
Kuzaliwa kwa ndama
Weka kumbukumbu sahihi na ufuatilie ng‘ombe mara nyingi zaidi wakati wanapokaribia kuzaa.
Ndama anaweza kuzaliwa wakati miguu ya mbele inatoka wanza kisha kichwa. Pia, anaweza kuzaliwa wakati miguu ya nyuma inatoka kwanza.
Ng‘ombe huhitaji msaada iwapo atachelewa kuzaa zaidi ya masaa 5.
Kulisha ndama
Ndama anapaswa kunyonya kutoka kwa mama angalau siku tatu, kisha tenganisha ng‘ombe kulingana na umri na anza kuwalisha maziwa kwa njia bandia.
Maziwa yanaweza kutolewe kwa kutumia chupa au ndoo.
Kati ya wiki 2 hadi 3 za umri walishe chakula cha wishwa, na pia wape chakula cha nyongeza. Unapotumia nyasi hakikisha kuwa ni za ubora wa juu, laini na zimechanganywa na kunde.
Mafunzo ya kibinafsi
Ndama hula hadi asilimia 10% ya uzito wa mwili wake kwa takriban wiki 6.
Kujihusisha na mbinu ya kujifunzia kupitia miradi ya mafunzo ya televisheni, hadithi za ukulima za kila siku katika magazeti na makala za mtandaoni ili kuboresha uzalishaji.