Kupitia ulishaji sahihi na mbinu bora za usimamizi, maganda bora ya mayai yanaweza kupatikana.
Ganda hutolea yai umbo sahihi ili kuhifadhi madini, na kulinda yaliyomo kwenye yai. Ganda la yai lina madini kama vile kalsiamu kaboneti, fosforasi, magnesiamu, viumbe hai, sodiamu, potasiamu, manganese, chuma na shaba.
Mambo yanayoathiri ubora wa ganda la yai
Muda na utoaji wa kalsiamu kwenye ganda, kadiri yai linavyochukua muda kwenye kwenye ganda ndivyo ganda linavyozidi kuwa nene.
Magonjwa; hupunguza ubora wa ganda la yai.
Umri wa ndege, kwa kawaida ganda la yai hudhoofika kadiri ndege anavyozeeka.
Dawa kama vile dawa za salfa, maji duni, ulaji wa chakula duni pia hupunguza ubora wa ganda la yai.
Kutunza ganda la yai
Hakikisha makazi sahihi na utunzaji sahihi wa mayai wakati wa kuyakusanya.
Hakikisha utayarishaji sahihi wa chakula cha kuku ili kuongeza kiwango cha kalsiamu.
Ongeza askobiki asidi kwenye chakula cha kuku kwa ajili ya kuboresha ganda la yai.
Mwishowe, lisha ndege kwa madini kama vile kalsiamu, manganese, shaba ili kuimarisha ganda la yai.