»Jinsi ya kuchagua eneo bora la mabwawa ya samaki«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Le3ufCWlDBc

Muda: 

00:08:40
Imetengenezwa ndani: 
2015

Imetayarishwa na: 

munalaFISH

Kwa uchaguzi sahihi wa eneo la mabwawa, pamoja na kuhakikisha uzingatiaji unaofaa, wakulima wanaweza kufaidika zaidi katika ufugaji wa samaki. Hata hivyo, uchaguzi duni husababisha changamoto kadhaa.

Vyanzo vya maji vya kawaida kwa mabwawa ya samaki ni pamoj na mito midogo, visima na maji kutoka kwenye paa. Funga ukuta wa bwawa ili kuzuia upotezaji wa maji, au tengeneza mabwawa ya zege.

Uchaguzi wa eneo

Chagua eneo lenye mwinuko wa ardhi uliyo teremka ili kuwezesha maji kutiririka ndani na nje ya bwawa.

Daima epuka maeneo tambarare kwa sababu haya huathiriwa na mafuriko wakati wa mvua kubwa.

Epuka maeneo yenye mwinuko sana, kwani yanahitaji kazi nyingi za ujenzi, na pia kuta zinaweza kuanguka wakati wa mvua kubwa.

Chagua eneo lisilo na mawe makubwa.

Udongo usiwe na kokoto nyingi,changarawe wala mchanga kwa kuwa vinahimiza upotevu wa maji.

Pia epuka udongo wa mfinyanzi kwa vile udongo hutoa nyufa ambazo husababisha upotevu wa maji.

Epuka maeneo yenye miti mikubwa ambayo inaweza kuenea hadi kwenye mabwawa na pia mizizi inaweza kuacha mapengo baada ya kuoza, ambazo hupitisha maji.

Epuka maeneo yenye mchwa kwa vile pia hutengeneza mashimo kwenye udongo na hivyo kupitisha maji.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua eneo

Zingatia usalama, soko na ufikiaji wa shamba ili wateja waweze kupata bidhaa kwa urahisi.

Pia zingatia gharama za kazi kwa ajili ya kupanga vizuri.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:22Masuala ya kuzingatia katika uchaguzi wa eneo la bwawa la samaki.
01:2201:54Chagua eneo lenye mwinuko wa ardhi uliyo teremka
01:5503:10Epuka maeneo tambarare
03:1104:24Chagua maeneo yenye maji safi, mengi yanayopatikana mwaka mzima.
04:2504:42Kinga bwawa kutokana na kupoteza maji mengi.
04:4305:12Chagua eneo lisilo na mawe makubwa.
05:1305:41Udongo usiwe na kokoto nyingi,changarawe wala mchanga
05:4206:41Epuka maeneo yenye miti mikubwa, mchwa na mizizi mikubwa.
06:4208:03Zingatia usalama, soko na ufikiaji wa shamba ili wateja waweze kupata bidhaa kwa urahisi

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *