Ingawa kuku hutoa nyama, mayai, kipato na samadi kwa wafugaji, wana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa. Ugonjwa wa kideri ndio muuaji mkubwa wa kuku.
Ugonjwa ukishatokea, hakuna tiba na hivyo huua kundi zima la kuku. Ugonjwa huu huathiri ubongo na mfumo wa upumuaji wa kuku, na mara baada ya kuathiriwa, shingo la ndege hujipinda na mabawa hupooza. Ugonjwa huu huenezwa na kuku wagonjwa na watu.
Udhibiti wa ugonjwa wa kideri
Kideri huzuiliwa tu na hutibiwi. Jinsi ya kuzuia kideri ni pamoja na kutenganisha kuku, na kuwachanja. Ufanisi wa chanjo huanza wiki moja baada ya kuchanja ndege. Katika hili, fuata maagizo ya mtengenezaji wa chanjo juu ya jinsi ya kutumia dawa. Unapotumia chanjo, ihifadhi kati ya nyuzijoto 2 hadi 8, na unaposafirisha chanjo shambani,tumia chombo kilicho na barafu ndani ili kudumisha ubaridi.
Vile vile, angalia maagizo yaliyoandikwa kwenye chupa ya chanjo. Kwa matumizi ya chanjo ya La Sota, epuka kuwapa maji kwa kuondoa vyombo vyote vya maji na kuwapa chakula kikavu. Kwa ufyonzaji bora wa chanjo ongeza unga wa maziwa kwenye lita tano za maji. Changanya chanjo kulingana na maagizo yaliyoandikwa kwenye chupa na katika hili, fungulia chupa ya chanjo ndani ya maji.
Gawanya maji yenye dawa katika vyombo tofauti na uviweke kwenye maeneo kadhaa. Chanjo yote iliyochanganywa inapaswa kupewa kwa ndege ndani ya masaa mawili. Hata hivyo, kwa chanjo 1–2 weka tone moja kwenye jicho la kuku, na katika siku za joto chanja ndege asubuhi au kwenye kivuli. Mimina chanjo iliyobaki kwenye choo, osha na kusafisha vyombo baada ya kuchanja. Chanja ndege kila baada ya miezi minne, na pia katika hali ya kuzuia ugonjwa.
Hatimaye, waondoe na uwatenganishe ndege wagonjwa ili wasichanganyike na wenye afya.