Afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa zinazozalishwa.
Kumfunga mnyama kabla ya kumpa chanjo ni vizuri kwa usalama wa binadamu na mnyama. Wakati wa kuchanja mnyanya, fuata maagizo yaliyo andikwa kwenye lebo ya dawa.
Kumdunga chanjo mnyama
Kwanza funga mnyama na tambua mahali pa kudunga sindano. Hata hivyo, sehemu maalum ya pembetatu iliyo kwenye shingo ndiyo inayopendekezwa zaidi kudungwa. Hifadhi chupa za dawa na sindano mahali penye baridi, pasipoingiza mwanga wa jua, na linda chanjo dhidi ya halijoto kali. Epuke kudunga mshipa wa shingo.
Vile vile zungusha chupa ili kuchanganya chanjo, na usiitikishe kwa nguvu kwani huku kunaweza kuharibu chanjo. Soma lebo ya bidhaa kila wakati ili kubaini kipimo kinachofaa.
Tumia kipimo sahihi cha chanjo. Tumia sindano mpya kuondoa chanjo kutoka kwa chupa, kwani sindano ambayo imetumiwa kwa wanyama inaweza kuchafua chanjo. Chagua sindano sahihi kwa kuzingatia njia ya kutoa chanjo, na uzito wa mnyama. Pindua chupa na shikilia bomba ya sindano kwa mkono mwingine na ingiza sindano ndani ya chupa.
Zaidi ya hayo, shikilia bomba ya sindano na chupa kwa mkono mmoja na tumia mkono mwingine kuondoa kipimo cha chanjo unachohitaji. Kisha chomoa sindano kutoka kwenye chupa huku ukielekeza juu, ondoa chanjo kidogo ili kuondoa hewa yoyote kwenye bomba au sindano, na hivyo kuhakikisha kipimo sahihi. Hakikisha mahali pa kudunga sindano ni safi, kavu na bila uchafu na utumie njia sahihi ya kudungaa chajo kama ilivyoorodheshwa kwenye lebo ya chanjo.
Kwa sindano ya chini ya ngozi, vuta ngozi ya shingo ya mnyama ili kuunda mahali pa kudunga sindano, toa chanjo, ondoa sindano na uiachie ngozi. Kwa sindano ya ndani ya misuli, dunga sindano kwenye misuli, ingiza chanjo na ondoa sindano.
Mwishowe, badilisha sindano mara kwa mara na utupe sindano zilizopinda na zilizoharibika.