Ufugaji wa kambare hutoa kipato kwa wafugaji na ni rahisi kuanzishwa, kwani huhitaji vifaa kidogo kama vile matangi ya kuhifadhia maji, chanzo cha maji, umeme na mirija.
Kuna faida kadhaa za ufugaji wa kambare kama vile, ni chanzo cha protini, hauhitaji uchimbaji wa vidimbwi, samaki hukomaa haraka, hula aina mbalimbali za malisho, hukua kwenye maji yenye hewa ya oksijeni kidogo, hustahimili msongamano mkubwa, huweza kuuzwa kwa njia mbalimbali, huhitajika sana na wateja, ni chanzo cha ajira na huhitaji mtaji mdogo.
Mambo ya kuzingatia
Daima lisha samaki kwa vyakula vyenye virutubishi vingi pamoja ili kufikia ukubwa na uzito bora wa samaki, pamoja na kudumisha afya bora.
Hakikisha unalisha samaki mara nyingi kwa siku, na pia chunguza samaki wanapokula ili kuhakikisha kwamba malisho yote yanatumiwa.
Tumia malisho ambayo hayatatengana katika maji ili kuepuka uchafuzi wa maji.
Tumia milisho ambayo yatakuwezesha kuwa na usimamizi wa ubora wa maji ili kuepuka kulisha samaki kupita kiasi, na pia kutoweza kutambua matatizo yanayohusiana ya ulishaji na milipuko ya magonjwa.
Chakula cha samaki
Chakula cha kuanzia, hiki kina viungo vilivyosawazishwa vizuri na hutolewa kwa kambare katika hatua ya awali ya ukuaji.
Chakula kinchoelea juu ya maji, hiki hutolewa kwa ajili ya hatua ukuaji na kina viungo vyote vinavyoweza kusaidia kunenepesha samaki na kuongeza uzito.
Chakula cha ukuaji, hiki kina kivutio ambacho huhimiza ulaji wa chakula, na hivyo kuharakisha ukuaji wa kambare.