Mojawapo ya vyanzo vya nyuki ni kuhamisha na kukamata kundi.
Kabla ya kuanza mchakato wa kuhamisha kundi, hakikisha kwamba una vifaa vyote muhimu vinavyohitajika ambavyo ni pamoja na kisanduku cha karatasi, shuka ya rangi isiyokolea, brashi ya nyuki, mkasi, mafuta ya nyasi ya limao, mavazi ya kujikinga na ngazi. Kundi linapokuwa karibu na ardhi, unaweza kulikuhamisha kwa urahisi lakini likiwa juu zaidi ya ardhi, unahitaji kutumia ngazi ili kulifikia.
Kuhamisha kundi la nyuki
Ili kuhamisha kundi la nyuki, tandaza shuka chini ya kundi na uweke kisanduku cha karatasi juu ya shuka. Ingiza nyuki ndani ya kisanduku na hakikisha malkia wa nyuki ameingia pia.
Ikiwa Malkia hakuingia kwenye kisanduku, subiri hadi nyuki wajikusanye tena na ujaribu tena. Ikiwa kundi la nyuki liko kwenye tawi, litikise tawi ili nyuki waanguke kwenye kisanduku. Ikiwa kundi linaning‘inia kwenye tawi dogo au mmea, tumia mkasi kukata tawi na uliweke kwenye kisanduku, lakini unahitaji kuondoa majani kabla ya kuweka nyuki kwenye mzinga mkuu.
Ikiwa kundi liko kwenye uzio/ukuta, unaweza kuhitaji nyunyizia nyuki maji ili kuwazuia kuruka. Ikiwa kundi liko chini, paka mafuta ya nyasi ya limau kwenye kisanduku na geuza kisanduku ili nyuki waingie ndani kwa urahisi
Kuingiza nyuki ndani ya mzinga
Baada ya kuhamisha nyuki wengi, funga kisanduku lakini acha upenyo mdogo ili nyuki wanaorejea waingie. Saa za usiku, funga kisanduku na ukimarishe kwa mkanda wa kuziba na usafirishe nyuki kwa upole.
Kisha inginza kundi kwenye mzinga na weka mbao za juu kisha ufunike mzinga.
Wafugaji wa nyuki wanaweza kutumia mafuta ya limau kuvutia makundi, lakini kisunduku kinapaswa kuinuliwa futi 6 kutoka ardhini.