Nyanya ni mboga zinazolimwa duniani kote kutokana na faida zake za kiafya. Hata hivyo nyanya huathiriwa na idadi ya wadudu na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika na kudhibitiwa kwa urahisi.
Magonjwa ya kawaida ya nyanya ni mnyauko wa bakteria, bakajani, batobato na ukungu. Wadudu waharibifu wa kawaida ni pamoja na vidukari, sota, dumuzi, wadudu chawa, inzi weupe, na viwavi, ambao wanapaswa kudhibitiwa ili kupata mavuno bora. Ili kufanikiwa na kilimo hiki, nyanya huhitaji nitrojeni, fosforasi, kalsiamu, potasiamu na magnesiamu. Nyunyiza na kemikali zenye viambato amilifu kama vile copper hydroxyl, metalayxl na mancozeb.
Kuhakikisha mavuno mengi
Epuka kuharibu mimea wakati wa kupalilia, kwani huku kunaweza kusababisha majeraha ambayo yanaweza kuwa sehemu za kuingilia magonjwa. Tumia matandazo ya plastiki, ambayo husaidia kupunguza athari za magugu. Weka mbolea kwa kiwango kinachopendekezwa baada ya kupalilia mara ya kwanza ili kurutubisha udongo.
Pima rutuba ya udongo kabla ya kupanda mimea ili kuangalia viwango vya virutubisho na kiwango cha pH. Dhibiti magonjwa na wadudu kwa mfano kwa kutumia maji yaliyotibiwa. Tibu udongo ili kuua wadudu na magonjwa yanayotokana na udongo. Weka kemikali zinazopendekezwa ili kudhibiti wadudu na magonjwa.
Panda mseto na badilisha mazao, palilia shamba, ondoa mimea yenye magonjwa, na dhibiti magonjwa mapema ili kuvunja mzunguko wa maisha ya wadudu na magonjwa. Hata hivyo, tumia kemikali zinazopendekezwa kila baada ya wiki 2 ili kuhakikisha udhibiti wa wadudu na magonjwa mapema. Vuna katika makundi kila wiki kwa mapato endelevu katika msimu mzima.