Nyanya hustawi vizuri kwenye maeneo ya joto, na ni mboga muhimu sana yenye faida kubwa kiafya. Hata hivyo, nyanya huhitaji udongo wenye rutuba na uwezo wa kuhifadhi maji na udongo unaopitisha maji kwa urahisi.
Kuna aina kadhaa za nyanya zenye sifa maalum, kwa mfano aina ambazo zina muda mfupi wa kuvunia na aina ambazo zina muda mrefu wa kuvunia. Unapopanda nyanya, kitalu kinapaswa kuinuliwa sm 15 juu ya ardhi ili kuzuia magonjwa yanayotokana na udongo, na kuwezesha upenyezaji mzuri wa maji.
Kanuni za kimsingi
Kila mara tumia aina za nyanya zilizoboreshwa, hii husababisha uhifadhi sahihi, hurahisisha usindikaji, na upinzani dhidi ya magonjwa. Hii pia husaidia wakulima kupata bei ya juu ya mazao. Kwa hivyo, panda nyanya moja kwa moja shambani au kwenye kitalu.
Weka kivuli juu ya kitalu ili kuzuia uvukuzi wa unyevu. Nyunyizia maji kila siku ili kuzuia kunyauka kwa mmea. Pima uotaji wa mbegu siku 8 baada ya kupanda. Kisha pandikiza mwezi 1 baada ya kupanda mbegu. Hata hivyo, panda ukiacha muda ya wiki 2 kati ya makundi ili kurahisisha uvunaji.
Pandikiza kwa uangalifu ili kuzuia uharibifu wa mazao na pia panda siku hiyo hiyo wakati miche inatolewa kwenye kitalu.
Ongeza mbolea oza au mboji kwenye udongo kulingana na rutuba ya udongo ili kurutubisha udongo. Miezi 2 baada ya kupandikiza, dhibiti magugu ili kupunguza ushindani wa virutubisho na madini.