Kupanda mboga kwenye magunia hutoa mavuno mengi kwa nguvu kidogo na muda mfupi. Hii ni chanzo mbadala cha mapato kwa wakulima kwa vile mboga kadhaa zinaweza kupandwa kwenye gunia moja. Mbinu hii inaweza kutumika katika misimu ya mvua na kiangazi.
Kuna nyenzo kadhaa zinazohitajika na hizi ni pamoja na mawe, udongo, majivu ya maganda, kinyesi cha ng‘ombe au kuku. Mawe husaidia kupunguza mgandamizo wa udongo na upenyezaji wa maji. Mianzi huokoa maji kwani hudhibiti uvujaji na uvukizi wa maji, na hivyo udongo hubaki na unyevu kwa siku moja au mbili. Fanya mzunguko wa mboga tofauti ili kuvunja mzunguko wa maisha ya magonjwa. Badilisha magunia mazee.
Kukuza mboga kwenye gunia
Kwanza, weka mawe chini ya gunia kwani haya husaidia kutiririsha maji na pia kulainisha udongo. Kisha changanya udongo, majivu na samadi vizuri. Weka nyasi kavu kwenye mawe, na ongeza udongo uliochanganywa kwenye magunia bila kuushinikiza.
Tengeneza mashimo madogo kwa umbali wa sm 10 kwenye bomba la mianzi katika muundo wa zig zag ili maji yatiririke kwa urahisi kwenye udongo. Kisha weka bomba la mianzi lenye mashimo katikati ya gunia huku ukiliinua sentimita 10 juu ili kuzuia maji kupenyeza ardhini.
Kupanda mboga kunapaswa kufanywa juu na kando ya magunia, kisha mwagilia maji kwenye bomba kila asubuhi, lakini mwanzoni mwaga maji moja kwa moja kwenye mimea na ndani ya bomba la mianzi kwa ukuaji mzuri wa mizizi.
Mboga zinapokua, vuta juu gunia ili kuongeza udongo. Panda mimea 4 hadi 5 kwa kila gunia kwa nafasi ifaayo ili kuwezesha ukuaji mzuri wa mimea. Ikiwa mimea itapandikizwa, kata majani kwa ukuaji sahihi wa mmea.