Mazao ya vitunguu yanaweza kuongezeka kwa kupandwa kwenye udongo wenye rutuba, kwa gharama ya chini. Rutuba ya udongo inaweza kuboreshwa kwa kutumia mbolea ya kikaboni au madini.
Vitunguu vinaweza kukuzwa kwenye udongo wa kichanga na udongo wa mfinyanzi kwa kutumia mbolea kama samadi au mbolea oza, kwaani hizi hutoa chakula cha mmea. Mbolea ya kikaboni huchanganywa na udongo angalau kina cha 10cm hadi 20cm ardhini.
Rutuba ya udongo
Nyunyiza maji ya kutosha, kwa sababu maji mengi huzamisha virutubisho chini kwenye udongo. Kufanya udongo kuhifadhi maji zaidi, ongeza mbolea ya kikaboni kabla ya kupandikiza miche ili mimea inawiri. Sambaza mbolea ya kikaboni iliyochanganywa na udongo wa juu, kwaani vitunguu vina mizizi ya kina kifupi.
Weka kwa uangalifu mbolea ya madini kama vile; Nitrojeni, fosforasi na potasiamu wiki 2 baada ya kupandikiza. Nitrojeni husaidia kutengeneza majani, Phosphorus hutengeneza mizizi, na Potasiamu husaidia mimea kustahimili na kuwa sugu dhidi ya magonjwa. Potasiamu inafaa kuongezwa katika udongo wakati wa kupalilia na wakati mmea unaonyesha dalili za upungufu wake.
Tumia mbolea za kemikali au madini kwa kiwango kidogo, kwa kufanya michimbuo midoga sana kati ya mistari ya mimea ili yaweze kufaidika sawa. Epuka kutumia urea miezi 2 kabla ya kuvuna, kwani nitrojeni nyingi hufanya vitunguu kuwa laini. Weka potasiamu au majivu ya kuni ili kuimarisha ngozi ya kitunguu. Mwishowe, weka samadi au mbolea oza ili kulainisha udongo kwaani kuwezesha upenyezaji bora wa maji, na ukuaji bora wa mimea.