»Jinsi ya kutengeneza kiota cha sungura na nini cha kufanya kabla na baada ya sungura kuzaa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=xThEr73XfhQ

Muda: 

00:15:56
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Best Farming Tips

Sungura waliozaliwa huwa dhaifu, kwa hivyo matayarisho yanapaswa kufanywa kabla sungura hajazaa.

Sungura anaweza kuanza kuzaliana akiwa na miezi 6 kwa aina kama vile New Zealand nyeupe na miezi 8 hadi 9 kwa aina kama vile chinchilla kubwa. Muda wa ujauzito wa sungura ni kati ya siku 28 hadi 30, lakini kawaida ni siku 21 na sungura huzaa kati ya mtoto 1 hadi 14 lakini kwa mara ya kwanza, atazaa kati ya 6 hadi 8. Mara ya kwanza sungura mama anaweza kushindwa kutunza watoto kwa hivyo unahitaji kuhakikisha kuwa wanatunzwa ipaswavyo kwa kuwatolea joto na chakula kizuri.

Maandalizi kabla ya kuzaa

Unapotarajia sungura kuzaa, unahitaji kuandaa viota na kuviweka kwenye banda la sungura takriban siku 5 kabla ya kuzaa. Kiota kinapaswa kuwa na urefu wa 35 cm, upana wa 25 cm, na urefu wa 12 cm juu. Baada ya kutengeneza kiota, weka maranda ya mbao sakafuni kwa ajili ya kuondoa unyevu, na pia weka nyasi kama matandiko.

Weka kihori cha maji mbali na kiota ili kuzuia sungura wachanga kuzama.

Baada ya sungura kuzaa, hakuna kitu cha kufanya kwa sababu sungura mama atawatunza watoto. Kagua viota na uondoe manyoya ili kuangalia kama tumbo la sungura limepanuka na kupunguka, walakini epuka kugusa sungura mtoto.

Ikiwa unapata sungura mtoto alie na tumbo iliyopungua, unahitaji kumlazimisha mama kumlisha. Ni kawaida kwa sungura kuzaa kati ya muachano wa siku 1 hadi 3.

Endelea kufuatilia na ikiwa utapata sungura aliyekufa, muondoe. Ikiwa chakula ni kichache, kuna tabia ya mama sungura kuua na kula watoto wake.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:49Sungura anaweza kuanza kuzaliana akiwa na miezi 6 hadi 9.
00:5001:25Muda wa ujauzito wa sungura ni kati ya siku 28 hadi 30, lakini kawaida ni siku 21.
01:2601:40Mara ya kwanza sungura mama anaweza kushindwa kutunza watoto
01:4101:50Weka maranda ya mbao kwenye kiota kwa ajili ya kuondoa unyevu, na pia weka nyasi kama matandiko.
01:5102:10Tengeneza viota na kuviweka kwenye banda la sungura takriban siku 5 kabla ya kuzaa
02:1103:06Ukubwa wa kiota
03:0703:15Weka kihori cha maji mbali na kiota.
031604:28Baada ya sungura kuzaa, kagua viota ili kuhakikisha kwamba sungura watoto wanatunzwa ipaswavyo.
04:2905:04Ikiwa unapata sungura mtoto alie na tumbo iliyopungua, unahitaji kumlazimisha mama kumlisha.
05:0506:20Ni kawaida kwa sungura kuzaa kati ya muachano wa siku 1 hadi 3.
06:2107:09Ikiwa chakula ni kichache, kuna tabia ya mama sungura kuua na kula watoto wake.
07:1015:39Mchakato wa kutrngeneza kiota
15:4015:56Hitimisho

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *