Kwa vile ulishaji unasalia kuwa mojawapo ya vipengele muhimu vinavyoathiri uzalishaji wa kuku, ubora wa malisho ni muhimu. Ubora huu huamuliwa na umri wa kuku, madhumuni ya uzalishaji na hatua ya ufugaji wa kuku.
Pia ubora huamuliwa na afya ya kuku. Wakati wa kutengeneza vyakula vya kuku, mahitaji yote muhimu ni lazima yawepo ili kuwa na chakula bora kilicho na lishe pamoja na uwiano sahihi.
Kutengeneza vyakula vya kuku
Tumia mahindi ya manjano kwa ubora wa sehemu ya ndani ya yai. Hii pia hupunguza vifo vinavyosababishwa na upungufu wa madini. Tumia mchanganyiko wa chokaa na ufuta kupata kiasi kikubwa cha nishati, na kupunguza mafadhaiko.
Vile vile, ongeza wishwa au pumba za mahindi na uzichanganye vizuri kwa kutumia sepetu, na kisha ongeza soya kwenye mchanganyiko huo. Mchanganyiko huo huwekwa kwenye mtambo na kuswaga.
Mwishowe, ongeza madini kwenye chakula kilichosagwa, na kisha ukichanganye ili kupata usawa wa chakula.