Kwa kawaida farasi huishi porini, hata hivyo kwa wafugaji wa farasi kuna baadhi ya mambo ya kimsingi ambayo yanapaswa kufanywa ili farasi wakue na afya.
Wafugaji wanapaswa kuwapa farasi nyasi bora ambazo zinaweza kumeng’enywa kwa urahisi kwani farasi humeng‘enya chakula tofauti na ng‘ombe. Zaidi ya hayo, kuna vifaa muhimu vya kimsingi ambavyo wafugaji wa farasi wanapaswa kuwa navyo kabla ya kununua mnyama na baadhi ya hivyo ni pamoja na kamba, brashi, kisafisha kwato, vifaa vya matibabu, dawa na blanketi.
Hatua za utunzaji
Watolee wanyama nyasi mbichi, nyasi kavu na viwango vya sukari vilivyosawazishwa, na nafaka bora kama chakula cha ziada, na pia shauriana na daktari wa mifugo.
Zaidi ya hayo, wape farasi maji ya kutosha ili kuzuia wanyama kukosa maji mwilini.
Acha farasi wawe nje katika uwanja mkubwa uliozungushiwa uzio ili waweze kutembea kwa urahisi na kulisha kwa uhuru.
Farasi wanaweza pia kufugwa kwenye banda, walakini ni muhimu kushauriana na daktari wa mifugo kuhusu mahali pa kufugia farasi kwa kuwa aina fulani za farasi zinaweza kuwekwa ndani wakati aina nyingine haziwekwi ndani.
Zaidi ya hayo, farasi wanaofugwa kwenye banda wanapaswa kuhamishwa nje mara moja kwa siku ili kuwawezesha kufanya mazoezi.
Hakikisha unasafisha chumba cha farasi kila siku ili kudhibiti magonjwa. Chunguza farasi, wasafishe, na pia kata kwato zao kila baada ya wiki 4 hadi 8 kulingana na hali ya hewa ili kudumisha afya yao.
Daima wape viatu kwa mfano wakati wa mbio, na chunguza mnyama kwa uangalifu kila siku ili kutambua kwa urahisi matatizo ya kiafya.
Mwishowe, hakikisha unawapa wanyama dawa ya kuua minyoo mara kwa mara ili kudumisha afya yao.