Asali ni moja wapo ya bidhaa muhimu katika ufugaji wa nyuki, na uvunaji sahihi wa asali ni muhimu katika kudumisha ubora wa asali.
Kabla ya kuingia kwenye safari ya kwenda kuvuna asali, vaa vaazi la kujikinga dhidi ya kuumwa na nyuki. Lazima uwe na kitoa moshi, brashi laini ya kuondoa nyuki kwenye masega, na kifaa cha kufungulia mzinga.
Uvunaji wa asali
Fungua mzinga wa nyuki na uangalie masega yaliyojazwa na asali. Acha masega yaliyojazwa nusu ili kuwawezesha nyuki kuyajaza asali kikamilifu. Baada ya kuondoa masega nje, funika tena mzinga.
Weka masega kwenye wilibaro (toroli) na uyafunike. Chukua masega kwenye chumba cha usindikaji ambapo asali huchimbwa kutoka kwenye masega na huchakatwa.
Ondoa safu ya juu ya nta kutoka kwa asali kwa kutumia kisu, na kisha weka masega yaliyo na asali kwenye zana ya kuchimba asali na uizungushe. Hii huondoa asali kutoka kwenye masega.
Baada ya kuzungusha, ruhusu asali kujikusanyia chini ya kifaa. Fungua bomba la kifaa ili kuruhusu asali kutiririka kupitia vichujio hadi kwenye ndoo. Kisha asali huwekwa kwenye chupa na kufungwa.