Kilimo mseto ni upandaji wa miti pamoja na mazao ya kawaida.
Kilimo cha miti kina faida kama vile kutoa kuni, samadi ya kijani kibichi, majani makavu kwa ajili ya mboji, malisho ya mifugo, chakula, na makazi ya ndege, chavua kwa n.k. Kukata miti iliyokomaa baadaye kunamletea mkulima pesa zaidi. Miti iliyochaguliwa kwa ajili ya kilimo mseto lazima iwe na uwezo wa kukua haraka, kunyooka na isiwe na matawi mengi, inapaswa kuwa na mfumo wa mizizi iliyo na kina kirefu ili kuzuia kushindania maji na virutubisho na mazao. Miti ya mikunde na mimea huongeza idadi ya viumbe hai, na ile yenye thamani ya kiuchumi inapewa kipaumbele katika mfumo wa kilimo mseto.
Miti ya kilimo mseto
Mtiki ni mti maarufu kwenye mipaka ya mashamba. Pogoa matawi ya kando ili kufanya mti uwe mrefu na unyooke vizuri. Kukata miti baada ya miaka 6 hadi 8 kutakuwezesha kupata kipato kikubwa na kuwezesha miti iliyobaki kukua vyema zaidi. Mtiki hausababishi matizo la kivuli kingi, na pia hutoa mbao muhimu baada ya miaka 25 hadi 30.
Subabul (Mlusina) ni mti muhimu wa kilimo mseto. Malisho yake yana viwango vingi vya protini, na hukua na kubadilika mti mkubwa katika miaka 6 hadi 8 tu. Pia hustahimili upogoaji wa matawi wa mara kwa mara kwa ajili ya kutoa malisho ya mifugo au mbolea ya kijani, na huenezwa kwa urahisi kwa mbegu.
Mwaloni wa fedha ni mti mmoja muhimu zaidi wa kilimo mseto unaotumika kwenye mipaka ya mashamba, na pia katika mashamba ya kahawa ili kutoa kivuli kidogo. Mbao kutoka kwa mwaloni wa fedha hupata bei nzuri kutokana na ubora wake.
Mkaratusi hupandwa kwenye mipaka na pia katika mashamba tofauti. Mikaratusi hutoa mashina yaliyonyooka ambayo ni muhimu kwa mbao na fito.
Miti ya malisho katika kilimo mseto ni pamoja na mgliricidia, mlindaziwa na mkaliandra. Katika mashamba ya kilimo mseto pekee, mazao ya msimu yanaweza kupandwa kati ya safu ya miti hadi miti itakapokuwa na mwavuli kamili.
Miti mingine ya kilimo mseto ni pamoja na mwarobaini, mkesia, mgunga na mikaratusi.