»Kilimo cha Mpunga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=dZ7tOCHb38g

Muda: 

00:13:21
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Ghana E-Agriculture

Mchele hutumiwa sana kwa sababu ya ongezeko la watu, ukuaji wa miji na mabadiliko ya upendeleo wa ya watumiaji. Hata hivyo, wakulima wengi wana maarifa kidogo ya mchakato wa uzalishaji wa mpunga.

Kuna faida kadhaa za kupalilia mpunga kama vile; kuhakikisha usafi wa aina, kupanua mazao, kuboresha mbegu na nafaka, na kupunguza asilimia ya nafaka zilizovunjika. Marekebisho ya kinu wakati wa kusaga hupunguza asilimia ya nafaka zinizovunjika.

Kilimo cha mpunga

Chagua eneo lenye udongo tifutifu au udongo wa mfinyanzi, lililo na chanzo cha maji kwa kukuza mpunga wa nyanda za chini, na udongo wa kichanga usio na maji mengi kwa mpunga wa nyanda za juu.

Lima ardhi ili kuhakikisha matumizi bora ya mbolea, kuongeza mianya ya hewa kwenye udongo, kurahisisha mbegu kuota na kudhibiti magugu.
Chagua mbegu bora zilizoidhinishwa na sifa zinazohitajika kama vile uwezo wa kutoa mazao mengi, kustahimili wadudu na magonjwa. 
Fanya vipimo vya uotaji, na panda kutegemea mbegu zilizoota. Iwapo zaidi ya 80% ya mbegu zitaota, panda mbegu 3 – 4, kwa 60 – 80% panda mbegu 5– 6 na iwapo chini ya 60% usipande mbegu hizo.
Safisha mbegu kwa kutumia maji ya chumvi na yai ili kuondoa makapi.
Panda mpunga kwenye vitalu vyenye unyevunyevu au vikavu na pandikiza miche kwa muda wa siku 21 katika umbali sahihi, na palilia shamba. 
Wiki 2 kabla ya kupanda weka magunia 140 – 160 ya samadi ya ng‘ombe au magunia 80 ya samadi ya kuku. Kwa hekta weka kilo 50 za samadi na uchanganye kwenye udongo ili kuongeza rutuba ya udongo. 
Palilia baada ya wiki 3 na 6 ili kupunguza ushindani wa virutubisho. 
Dhibiti wadudu na magonjwa ya mpunga kwa kukuza aina sugu na kudumisha usafi wa shamba.
Mwisho, kagua, vuna wakati 80% ya matawi ya mpunga yamegeuka kahawia. Kusanya na rundika mpunga, kisha pura.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:30Mchele hutumiwa sana kwa sababu ya ongezeko la watu
01:3101:35Kilimo cha mpunga
01:3601:56Chagua eneo lenye udongo tifutifu au udongo wa mfinyanzi, lililo na chanzo cha maji kwa kukuza mpunga wa nyanda za chini
01:5702:57Kwa mpunga wa nyanda za juu chagua udongo wa kichanga usio na maji mengi.
02:5803:39Tayarisha ardhi kwa kulima na kulainisha udongo.
03:4004:40Chagua mbegu bora zilizoidhinishwa na sifa zinazohitajika
04:4105:44Fanya vipimo vya uotaji, na panda kutegemea mbegu zilizoota
05:4506:37Safisha mbegu kwa kutumia mbinu ya maji ya chumvi
06:3808:39Panda mpunga kwenye vitalu vyenye unyevunyevu au vikavu na pandikiza miche kwa muda wa siku 21 katika umbali sahihi.
08:4010:32Wiki 2 kabla ya kupanda weka magunia 140 – 160 ya samadi ya ng‘ombe au magunia 80 ya samadi ya kuku. Kwa hekta weka kilo 50 za samadi na uchanganye kwenye udongo.
10:3311:10Dhibiti wadudu na magonjwa ya mpunga
11:1112:33Dhibiti wadudu na magonjwa ya mpunga
12:3413:21Kagua shamba, vuna wakati 80% ya matawi ya mpunga yamegeuka kahawia.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *