Aina kadhaa za nyanya zinaweza kupandwa kwa urahisi katika chafu. Hii inahakikisha kwamba mazao yanapatikana kwa mwaka mzima kwa bei nafuu.
Kupanda nyanya kwenye chafu kuna faida kadhaa kama vile; nyanya haziathiriki sana na mabadiliko ya hali ya hewa, na hivyo kuhakikisha ugavi wa mara kwa mara sokoni, pia hupunguza gharama za uzalishaji kwa vile kunahitaji kazi kidogo, na pia hupunguza matukio ya magonjwa. Pia tija ya ardhi katika chafu ni kubwa ikilinganishwa na kilimo shambani. Umwagiliaji wa kutonesha unapendekezwa kwani kumwagilia kupita kiasi husababisha uozo na kupasuka kwa matunda.
Kuongezeka kwa mapato
Hatua ya kwanza ya kuhakikisha mapato ya juu kutoka kwa chafu ni kwa kuandaa kitalu chenye upana wa mita 1, na kupanda mbegu kwa umbali wa sm15 kati ya safu, na sm 2 kati ya mbegu. Pia, mbegu zinaweza kuoteshwa kwenye trei.
Kila mara panda mbegu zilizochanjwa na dawa za kuua ukungu ili kuepuka mashambulizi ya wadudu na kuzuia munyauko. Chunguza miche na nyunyizia dawa ya kuua wadudu na magonjwa, punguza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupandikiza ili kufanya miche kuwa migumu.
Weka dawa za kuua minyoo fundo na wadudu wengine kabla ya kupandikiza ili kudhibiti wadudu waharibifu wa udongoni. Pandikiza miche baada ya siku 18 hadi 21. Wakati wa kupanda hakikisha umbali wa sm 60 kwa sm 45 kwani hii husababisha mavuno mengi na pia hurahisisha udhibiti wa wadudu na magonjwa. Fanya mzunguko wa mazao ili kuvunja mzunguko wa maisha ya ugonjwa na vile vile kuweka mbolea baada ya kupima udongo. Pia weka mboji ili kuongeza rutuba ya udongo.
Panda katika safu ili kupunguza msongamano wa mboga na hivyo kudumisha upenyezaji mzuri mzuri wa hewa ndani ya chafu. Mwagilia mimea lakini epuka kunyunyizia majani moja kwa moja ili kupunguza ukuaji wa magonjwa ya majani. Dhibiti magugu na weka fito za kuthibitisha miche baada ya kupandikiza. Pogoa ili kuimarisha ukuaji wa mimea. Nyunyizia dawa ili kuboresha maua. Chunguza mara kwa mara ili kushughulikia mmea iwezekanavyo.
Shusha chini mashina ya mimea mirefu ili kushughulikia mmea kwa urahisi, na kuvuna vizuri. Fungua madirisha ya chafu ili kusababisha upenyezaji mzuri wa hewa katika siku za joto. Funga madirisha wakati wa kibaridi ili kuondoa unyevu wa ziada. Vuna kwa wakati sahihi. Unaweza kushiriki mazao pomoja na wakulima wengine ili kupunguza gharama za usafiri na kuongeza faida.